Makala Mpya

14 wauawa, kujeruhiwa katika shambulizi karibu na ubalozi wa US, Kabul.

Habari kutoka Afghanistan zinasema, kwa akali watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia shambulizi la bomu lililotokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Kabul hii leo. Basir Mujahid, msemaji wa Mkuu wa Polisi mjini Kabul amesema, bomu hilo limeripuka nje ya benki mjini Kabul karibu na ubalozi wa Marekani, ambapo watu tisa pia wamejeruhiwa. [&hellip

Sierra Leone: Idadi ya wahanga wa maporomoko ya udongo imepita elfu moja.

Serikali ya Sierra Leone imetangaza kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo yaliyoambata na mafuriko katika mji wa milimani wa Regent nje kidogo ya Freetown imepindukia elfu moja. Maafisa wa serikali ya Sierra Leone wamesema kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maafa hayo imepindukia elfu moja hususan kwa kutilia [&hellip

JPM: Takukuru chukueni hatua kwa wala rushwa.

Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. Dk Magufuli alitoa kauli hiyo jana alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa Takukuru katika ofisi za Makao Makuu ya taasisi hiyo jijini Dar [&hellip

Wenger awataka mashabiki kudumisha imani baada ya kichapo Anfield.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani baada ya kile alichosema kuwa ni uchezaji wa kusikitisha sana baada ya klabu hiyo kucharazwa na Liverpool 4-0 katika mechi ya Ligi ya Premia Jumapili. Gunners hawakuwa na kombora hata moja lililolenga goli baada ya uchezaji mbaya ambao ulikosolewa pakubwa na [&hellip

Lipuli yaiduwaza Yanga.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga jana iliduwazwa na Lipuli kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi yake ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Matokeo hayo hayakutarajiwa na wengi kutokana na ugeni wa Lipuli kwenye ligi na hivyo iliingia uwanjani ikiwa haipewi nafasi ya kushinda. Lipuli iliyopanda Ligi Kuu [&hellip

CCM Yafuta Uchaguzi Kata 41 Kwa Mchezo Mchafu.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kupeleka salamu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali, wanaokiuka Katiba na Kanuni za Uchaguzi, baada ya kufuta uchaguzi wa ndani ya chama hicho katika kata 41 kati ya kata 4,420 zinazoshiriki katika uchaguzi huo, kutokana na kubaini mchezo mchafu na kuagiza mchakato kurejewa upya. Hayo yalibainishwa jana Dar es Salaam na [&hellip

Samia: Wekeni Masharti Nafuu Mikopo Ya Wanawake.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezitaka taasisi za kifedha pamoja na benki kuwa na masharti mepesi na maalumu ya mikopo kwa wanawake wajasiriamali wadogo. Amesema inashangaza kuona riba kubwa kwenye mikopo lakini kwenye amana riba, ikiwa ni ndogo na kuagiza uongozi katika benki zote nchini, kufanya kazi kwa maendeleo ya watu wote. Katika hatua [&hellip

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani akosoa matamshi ya kibaguzi ya rais wa nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amekosoa matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo. Rex Tillerson ambaye alikuwa akizungumza na televisheni ya Fox News kuhusu matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani juu ya matukio ya Charlotteville, amesema kuwa Trump anazungumza kwa niaba yake mwenyewe. Awali pia [&hellip

Al Azhar yalaani mauaji ya Waislamu wa Rohingya, Myanmar.

Taasisi ya Al Azhar nchini Misri imelaani vikali mauaji yanayoendelea kufanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wa Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo. Taafrifa iliyotolewa na Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri imesema kuwa, mauaji hayo dhidi ya Waislamu wa Rohingya yanapingana na mafundisho ya dini zote. Taarifa hiyo ya [&hellip

UN: Watu milioni 3.8 wamefurushwa makwao kutokana na machafuko DRC.

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na machafuko na mapigano nchini humo imeongezeka maradufu. George Okoth-Obbo, afisa katika Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR jana Jumamosi alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita, wakimbizi wa Kongo DR wameongezeka na kupindukia milioni [&hellip