Makala Mpya

Kikosi cha Hapa Kazi Tu 2015.

Kikosi cha Hapa Kazi Tu 2015.

      Rais John Magufuli ametangaza Baraza jipya la Mawaziri, ambalo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, ndio baraza lenye idadi ndogo ya wizara na mawaziri wake. Baraza hilo lilitangazwa jana Ikulu Dar es Salaam, lina jumla ya wizara 18, zenye mawaziri 19, ambapo kati ya hao, wizara nne hazijapata mawaziri, huku [&hellip

‘Serikali izibe pengo la uhaba wa madaktari’

‘Serikali izibe pengo la uhaba wa madaktari’

    Rais mstaafu, Alhaji Hassan Mwinyi (pichani), ameshauri serikali kufanya jitihada kubwa kuhakikisha inaziba pengo la uhaba wa madaktari na wauguzi kuokoa afya za Watanzania. Alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afya na Teknolojia (IMTU), yaliyofanyika chuoni hapo.   Katika mahafali hayo [&hellip

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Rwanda Akamatwa.

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Rwanda Akamatwa.

    Marekani inasema kuwa mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika pakubwa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, amekamatwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ladislas Ntaganzwa, ambaye ni meya wa zamani, anatuhumiwa kwa kuwaua maelfu ya watu na kupanga ubakaji wa jumla mwaka huo wa 1994. Ni mmoja kati ya washukiwa tisa wakuu wanaosakwa [&hellip

Magufuli atangaza baraza la mawaziri.

Magufuli atangaza baraza la mawaziri.

      Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa sasa lina mawaziri 19, ingawa wizara ni 18. Mawaziri sita kati ya hao ni wanawake. Dkt Magufuli amesema kuna nafasi nne za uwaziri ambazo bado anatafuta watu wanaofaa kuteuliwa. Walioteuliwa ni: 1.Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora. [&hellip

Marekani kupeleka helikopta za mashambulizi Iraq

Marekani kupeleka helikopta za mashambulizi Iraq

​Marekani imesema itapeleka washauri na helikopta za mashambulizi iwapo itaombwa kufanya hivyo na Iraq, ili kuukomboa mji wa Ramadi kutoka kwa wapiganaji wa kundi lenye itikadi kali la Dola la Kiislamu-IS.  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ulinzi, Ash Carter wakati akizungumza na kamati ya bunge ya masuala ya silaha. Amesema imechukua muda mrefu sana [&hellip

Watuhumiwa wa ugaidi wakamatwa Australia

Watuhumiwa wa ugaidi wakamatwa Australia

​Watu wawili wamekamatwa leo kwenye mji wa Sydney nchini Australia kwa tuhuma za kupanga kulishambulia jengo la serikali.  Vijana hao wamekamatwa kwenye nyumba zao mjini Sydney na wamefunguliwa shtaka moja moja kwa njama za kupanga na kutekeleza vitendo vya kigaidi. Watu wengine watatu wako gerezani na pia wanatarajiwa kushtakiwa kwa kosa kama hilo. Naibu Kamishna [&hellip

Watu 50 wauawa Afghanistan

Watu 50 wauawa Afghanistan

​Mpiganaji wa mwisho kati ya wapiganaji 11 wa Taliban ambao waliuzingira uwanja wa ndege wa Kandahar, Afghanistan ameuawa, zaidi ya saa 24, baada ya shambulizi kuanzishwa.  Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imesema leo kuwa watu 50 wakiwemo raia na maafisa wa usalama, wameuawa. Shambulizi hilo ambalo ni kubwa dhidi ya kambi ya jeshi la anga [&hellip

Jarida la Time: Markel shakhsia wetu wa mwaka

Jarida la Time: Markel shakhsia wetu wa mwaka

​Jarida la Time la nchini Uingereza limemtaja kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa shakhsia maarufu wa gazeti hilo kwa mwaka huu.  Jarida hilo limemtaja Abu Bakr al-Baghdadi mkuu wa genge la kigaidi la Daesh kuwa mtu wa pili wa gazeti hilo kwa mwaka huu kutokana na vitendo vyake vya kigaidi. Televisheni ya al Alam imelinukuu shirika [&hellip

Putin na Cameron wazungumzia Syria

Putin na Cameron wazungumzia Syria

​Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron wamezungumzia juu ya hali ya nchini Syria kwa njia ya simu.  Msemaji wa Ikulu ya Urusi ameeleza kuwa nchi mbili hizo zinalenga shabaha ya pamoja katika kupambana na magaidi wa dola la kiislamu na makundi mengine ya magaidi nchini Syria na katika kanda [&hellip

Wapinzani wa al- Assad wakutana Saudi Arabia

Wapinzani wa al- Assad wakutana Saudi Arabia

​Wajumbe zaidi ya 100 wa vyama vya upinzani vya nchini Syria, pamoja na pande mbalimbali za waaasi, pia kutoka makundi yenye msimamo mkali, wanakutana mjini Riyadh, kwa lengo la kuleta umoja wa wapinzani,wakati ambapo jumuiya ya kimataifa inashinikiza juu ya kuleta suluhisho la kisiasa ili kuumaliza mgogoro wa nchini Syria.  Makundi mbalimbali ya waasi zaidi ya [&hellip