Makala Mpya

Moyes awalalamikia waamuzi England

  Meneja wa Manchester United, David Moyes amedai kuwa timu yake inacheza dhidi ya waamuzi pamoja na timu pinzani baada ya kushuhudia vijana wake wakipoteza mchezo dhidi ya Sunderland katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Capital One. Kocha huyo wa Manchester United alisikitishwa na uamuzi wa kuipatia Sunderland penalti na hivyo kuiwezesha kuibuka [&hellip

Puntland yapata Rais Mpya

Puntland yapata Rais Mpya

  Wabunge katika jimbo la Puntland nchini Somalia wamemchagua waziri mkuu wa zamani wa Somalia Abdiweli Muhammad kama Rais mpya wa jimbo hilo linalojitawala ingawa linasema liko chini ya Somalia. Abdiweli, alimshinda Rais Abdirahman Muhammad Farole kwa kura 33 kwa 32 katika duru ya tatu na ya mwisho kutokana na wagombea kukosa kupata zaidi ya [&hellip

Uraibu wa sigara wawavutia wengi

Uraibu wa sigara wawavutia wengi

Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya. Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa na tabia hiyo. [&hellip

S.Kusini yakaribia kukomboa mji wa Bor

S.Kusini yakaribia kukomboa mji wa Bor

Serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa vikosi vyake vimekaribia kuukomboa mji wa Bor kutoka kwa waasi, huku mazungumzo ya kusaka amani kati ya pande mbili yanayofanyika huko Addis Ababa yakiripotiwa kupiga hatua kwa mwendo wa kinyonga. Taarifa iliyotolewa na afisa wa serikali ya Juba imeeleza kuwa, yamebaki masaa machache na vikosi vya SPLM vitatangaza kukombolewa [&hellip

Silaha za kemikali zaanza kuondolewa Syria

Silaha za kemikali zaanza kuondolewa Syria

Serikali ya Syria imeanza kuondoa mada za silaha za kemikali katika nchi hiyo zoezi ambalo halikuanza kwa muda wake uliopangwa kutokana na vita na matatizo ya kiufundi. Shughuli hiyo inasimamiwa na Taasisi ya Kuzuia Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPWC) ambayo imeeleza kuwa, mada hizo zinaondolewa katika Bandar ya Latakia nchini Syria na kupakiwa kwenye [&hellip

Kongamano la kupinga Uzayuni Tunisia

Kongamano la kupinga Uzayuni Tunisia

Kongamano la kimataifa la kuunga mkono muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel limeanza leo katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis. Wanazuoni wa Kiarabu, wanasiasa, wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wanaharakati wanashiriki kwenye kongamnao hilo la siku mbili lililoanza leo, ikiwa ni wiki moja kabla ya kuadhimisha mwaka wa 3 tangu kujiri  harakati za [&hellip

Loga: Washambuliaji wangu Simba butu

Loga: Washambuliaji wangu Simba butu

Kocha wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic ameitolea uvivu safu yake ya ushambuliaji na kubainisha kuwa imekuwa butu katika mashindano yanayoendelea visiwani hapa ya Kombe la Mapinduzi. Simba imecheza mechi zote tatu za Kundi B lililokuwa pia na timu za KCC ya Uganda, KMKM ya Unguja na AFC Leopards ya Kenya huku ikiambulia mabao mawili pekee [&hellip

Mama yake Dk. Mgimwa atoa ya moyoni

Mama yake Dk. Mgimwa atoa ya moyoni

Mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mbunge wa Kalenga Consolatha Semgovano, mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha na mbunge wa Kalenga, mkoani Iringa, marehemu Dk.William Mngimwa, amevunja ukimya kuhusu kifo cha mwanaye akisema kuwa moyo wake unasononeka na umepoteza amani kwa sababu haoni ni nani katika familiya yake atakayeweza kuwa mbadala wake [&hellip

Mbunge awaasa madiwani kusimamia miradi

Mbunge awaasa madiwani kusimamia miradi

Betty Machangu, Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro Madiwani na viongozi wengine katika halmashauri ya Moshi Vijijini wametakiwa kusimamia kikamilifu miradi inayotolewa na halimashauri pamoja na serikali kuu. Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu, alisema kumekuwa na usimamizi mdogo wa miradi vijijini kutokana na uzembe wa madiwani na viongozi [&hellip

Waziri Chiza asimamisha kazi kigogo

Waziri Chiza asimamisha kazi kigogo

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza, amemsimamisha kazi mrajisi wa mkoa wa Ruvuma, Watsoni Nguniwa, kwa kushindwa kutatua kero zinazowakabili wakulima wa mkoa huo. Akitoa agizo hilo jjijini Dar es salaam Waziri Chiza alisema wakati umefika kwa watendaji wote wa wizara yake ambao watashindwa kwenda na kasi ya sheria mpya ya mwaka 2013 [&hellip