Makala Mpya

Iran Itatoa Jibu Kali Kwa Magaidi Wanaopania Kufanya Mashambulizi Nchini.

Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu kali zaidi kwa magenge ya kigaidi yatakayojaribu kuleta chokochoko na kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya nchi hii. Rais Rouhani aliyasema hayo jana Jumanne hapa mjini Tehran akiashiria shambulizi la kombora lililofanywa hivi karibuni na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC dhidi [&hellip

Maandalizi Ya Kombe La Chan Yachelewa Kenya.

Haikuwa rahisi kwa Kenya kushinda haki za kuandaa kombe la matiafa ya Afrika 2018 Chan ambayo sasa yanawaponyoka. Shirikisho la soka nchini humo FKF likiongozwa na aliyekuwa katibu wake Sam Nyamweya lilitumia shilingi milioni 50 mwaka 2013 kupigania zabuni ya kuandaa michezo hiyo mbali na kusimamia safari za mara kwa mara za kuelekea makao makuu [&hellip

Jose Mourinho Adaiwa Kukwepa Kodi Uhispania.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametuhumiwa kufanya ulaghai wakati wa ulipaji kodi alipokuwa katika klabu ya Real Madrid. Maafisa wa mashtaka nchini humo wanasema alitenda makosa hayo alipokuwa mkufunzi mkuu wa klabu hiyo. Anatuhumiwa kukwepa kolipa kodi ya jumla ya €3.3m (£2.9m; $3.6m) kati ya mwaka 2011 na mwaka 2012. Bado hajazungumzia madai hayo. [&hellip

Zarif: Hakuna Kizuizi Cha Kuimarisha Uhusiano Wa Iran Na Tunisia.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hakuna kitu kinachoweza kuzuia au kukwamisha kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Iran na Tunisia. Mohammad Javad Zarif aliyasema hayo jana Jumatatu katika mazungumzo yake na Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi katika mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, Tunis. [&hellip

Larijani: Hatua Zote Za Saudia Ni Kwa Maslahi Na Manufaa Ya Israel.

Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameukosoa vikali utawala wa Aal-Saud kwa kushirikiana kufa kupona na utawala wa Kizayuni wa Israel na kubainisha kuwa, hatua zote za Riyadh katika eneo hili ni kwa maslahi na manufaa ya Tel Aviv. Ali Larijani aliyasema hayo jana Jumatatu hapa mjini Tehran katika mkutano na [&hellip

Rais Kuzindua Viwanda Vitano Pwani.

Rais John Magufuli leo anaanza ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Pwani na anatarajia kuzindua viwanda vitano. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam jana, katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua viwanda vikubwa vitano ambavyo ni kiwanda cha vifungashio (Global Packaging Co. Ltd) na kiwanda [&hellip

Binti Wa Kiislamu Auawa kikatili Jatika Jimbo La Virginia Nchini Marekani.

Polisi nchini Marekani imetangaza kuwa msichana mmoja wa Kiislamu ameuawa katika shambulizi lililofanywa na mtu mwenye chuki dhidi ya dini ya Uislamu katika jimbo la Virginia. Binti huyo wa kiislamu aliyekuwa na umri wa miaka 17 kwa jina la Nabra Hassanen, aliuawa Jumapili iliyopita baada ya kutoka msikitini katika jimbo hilo ambapo alitekwa nyara na [&hellip

Kamusi Kuu Ya Kiswahili Yazinduliwa Tanzania.

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali yake inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa taifa na katika kulinda umoja wa kitaifa. Ametoa kauli hiyo alipozungumza na wabunge, viongozi wa Serikali na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. “Serikali inatambua umuhimu wa [&hellip

Rugemerila, Singh Kortini Kwa Uhujumu Uchumi.

Wafanyabiashara wawili, James Rugemarila na Harbinder Singh Sethi walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana, wakikabiliwa na mashitaka sita ya uhujumu uchumi, likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani milioni zaidi ya 22 sawa na Sh bilioni 309. Rugemarila ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing [&hellip

Kwa Akali Watu 16 Wauawa Katika Shambulio La Kujiripua, Kaskazini Mwa Nigeria.

Habari kutoka Nigeria zinaarifu kwamba, kwa akali watu 16 wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa, katika mashambulizi kadhaa ya kujiripua kwa mabomu katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Polisi ya jimbo la Borno limetangaza kuwa, mashambulizi hayo ya kigaidi yametekelezwa na wanawake watano katika mji wa Maiduguri, makao makuu ya jimbo hilo la Borno. [&hellip