Category: This Day in History

Jumatatu, Juni 30, 2014

Jumatatu, Juni 30, 2014

Siku kama ya leo miaka 54 iliyopita mwafaka na leo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire) ilijitangazia uhuru wake na Joseph Kasavubu akawa rais wa nchi hiyo, huku Patrice Lumumba akiwa Waziri Mkuu. Kongo ilikoloniwa na Ubelgiji. Mapambano ya kudai uhuru yaliyoongozwa na Patrice Lumumba yalishika kasi katika miaka ya mwisho ya kumalizika kwa Vita [&hellip

Jumamosi, Juni 28, 2014

Jumamosi, Juni 28, 2014

Siku kama ya leo miaka 100 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 28 Juni 1914 aliuawa Franz Ferdinand mrithi wa kiti cha ufalme wa Austria akiwa pamoja na mkewe, wakati alipokuwa safarini Sarayevo, mji mkuu wa Bosnia Herzegovina ya leo, baada ya kufyatuliwa risasi na mwanachuo mmoja wa Kiserbia. Mara baada ya kutokea shambulio hilo, serikali ya [&hellip

Ijumaa, Juni 27, 2014

Ijumaa, Juni 27, 2014

Tarehe 6 Tir miaka 33 iliyopita Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ambaye wakati huo alikuwa mwakilishi wa Imam Ruhullah Khomeini katika Baraza Kuu la Ulinzi na pia Imam wa Ijumaa wa Tehran, alinusurika jaribio la kutaka kumuua lililofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la MKO. Magaidi hao walilipua bomu katika [&hellip

Alkhamisi, 26 Juni, 2014

Alkhamisi, 26 Juni, 2014

Siku kama ya leo miaka 760 iliyopita alizaliwa Marco Polo, mfanyabiashara na mtalii mashuhuri wa Kiitalia huko katika mji wa Venice. Baba na mjomba wa Marco Polo walikuwa miongoni mwa watalii mashuhuri wa Italia ambao walifanya safari huko Uchina ya Kaskazini, Mongolia, Turkistan ya Mashariki na Iran, nchi ambazo wakati huo zilikuwa chini ya utawala [&hellip

Jumatano, Juni 25, 2014

Jumatano, Juni 25, 2014

Siku kama ya leo miaka 192 iliyopita kundi la watumwa wa Marekani wenye asili ya Kiafrika ambao waliachiwa huru na wamiliki wao wazungu wa nchi hiyo, walirejea Afrika na kuanzisha makazi katika ardhi ambayo leo hii inajulikana kama Liberia. Raia hao weusi wa Marekani walianzisha harakati ya ukombozi mwanzoni mwa karne ya 19 kwa lengo [&hellip

Jumanne, Juni 24, 2014

Jumanne, Juni 24, 2014

Siku kama ya leo miaka 171 iliyopita, tanuu za feleji maarufu kwa jina la tanuu za Bessemer zilivumbuliwa. Mvumbuzi wa tanuu hizo alikuwa Mwingereza Henry Bessemer. Tanuu hizo zilitumika huko Uingereza kwa mara ya kwanza na leo hii zinatumika katika masuala mbalimbali viwandani. Tarehe 24 Juni miaka 202 iliyopita, Caracas mji mkuu wa Venezuela ulidhibitiwa [&hellip

Jumatatu, Juni 23, 2014

Jumatatu, Juni 23, 2014

Siku ya leo miaka 478 iliyopita, ilianza harakati ya kiongozi wa kidini na mpenda mageuzi wa Ufaransa Calvin John huko Geneva mji mkuu wa Uswisi. Alizaliwa mwaka 1509 Miladia na kujifunza sheria na masomo ya kidini. Katika zama za ujana wake, Calvin John alijiunga na harakati ya Kiprotestanti ilioasisiwa na Martin Luther. Aliivamia Geneva Uswisi [&hellip

Ijumaa, Juni 20, 2014

Ijumaa, Juni 20, 2014

Siku kama ya leo miaka 102 iliyopita msomi wa Poland kwa jina la Casimir Funk kwa mara ya kwanza kabisa alifanikiwa kugundua vitamin au virutubisho. Baada ya uhakiki mwingi Daktari Casimir Funk aligundua kwamba vyakula vinavyotumiwa na mwanadamu vina baadhi ya virutubisho (vitamin) ambavyo japokuwa ni vichache sana lakini vina udharura mkubwa katika ukuaji na [&hellip

Jumatatu, 16 Juni, 2014

Jumatatu, 16 Juni, 2014

  Siku kama ya leo miaka 7 iliyopita, alifariki dunia Ayatullahil-Udhma Sheikh Muhammad Fadhil Lankarani aalim na marjaa mkubwa wa Kiislamu baada ya kuugua. Allamah Fadhil Lankarani alizaliwa mwaka 1310 Hijria Shamsia katika mji wa kidini wa Qum huko kusini mwa Tehran na kuanza kujifunza masomo ya dini akiwa kijana mdogo. Aidha alipata kustafidi na [&hellip

Ijumaa, 13 Juni, 2014

Ijumaa, 13 Juni, 2014

Siku kama ya leo miaka 1180 iliyopita yaani tarehe 15 Shaaban mwaka 255 Hijria alizaliwa mwana wa Imam Hassan Askari ambaye ni miongoni mwa wajukuu watukufu wa Mtume wetu Muhamamd (saw) Mahdi (af) katika mji wa Samarra nchini Iraq. Miaka mitano ya mwanzoni Mahdi (as) aliishi na baba yake na kuchukua hatamu za uongozi wa [&hellip