Category: Mengineyo

Jumatano, Januari 23, 2013

Jumatano, Januari 23, 2013

Siku kama ya leo miaka 63 iliyopita, inayosadifiana na 23 Januari 1950, Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel liliutangaza mji wa Baitul Muqaddas, Kibla cha kwanza cha Waislamu, kuwa mji mkuu wa utawala huo. Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kupita miaka miwili tokea kuanzishwa utawala huo ghasibu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. [&hellip

Jumanne, Januari, 22, 2013

Jumanne, Januari, 22, 2013

Siku kama ya leo miaka 1462 Hijria miaka 28 kabla ya Hijra, Mtukufu Mtume Muhammad (saw) alimuoa Bibi Khadija binti Khuwailid AS. Bibi Khadija alikuwa mwanamke sharifu, mwenye imani na maarufu kwa ukarimu wake katika zama za ujahilia na alikuwa maarufu kwa lakabu ya “Twahira” kwa maana ya msafi na mtoharifu. Baada ya kufunga ndoa [&hellip

Jumatatu, January 21, 2013

Jumatatu, January 21, 2013

Siku kama ya leo miaka 1174 iliyopita baada ya kuuawa shahidi Imam Hassan Askari (as) kilianza rasmi kipindi cha uongozi wa Imam wa Zama Mahdi Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake. Imam Mahdi ni mwana wa Imam Hassan Askari (a.s) na miongoni mwa wajukuu wa Bwana wetu Muhammad (saw). Imam Mahdi yuko ghaiba kwa amri ya [&hellip

Jumamosi, Januri 19, 2013

Jumamosi, Januri 19, 2013

Siku kama ya leo miaka 34 iliyopita, wimbi na furaha, nderemo na vifijo lilitawala nchini Iran baada ya kuenea habari ya kukaribia kurejea nchini Imam Khomeini akitokea uhamishoni huko Ufaransa. Kila kona habari ya kurejea nchini Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na jinsi atakavyopokelewa ndio mambo yaliyotawala katika vinywa na ndimi [&hellip

Ijumaa, Januari 18, 2013

Ijumaa, Januari 18, 2013

Siku kama ya leo miaka 94 iliyopita yaani 18 Januari 1919, ulifanyika mkutano wa kihistoria wa amani baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, kwa kuwashirikisha wawakilishi wa nchi 27 kutoka mabara yote matano duniani. Nchi tano zilizoshindwa kwenye Vita vya Kwanza vya Dunia yaani Ujerumani, Austria, Hungary, Bulgaria na dola la Othmania, hazikushiriki kwenye [&hellip

Alkhamisi, 17 Januari, 2013

Alkhamisi, 17 Januari, 2013

Siku kama ya leo miaka 4 iliyopita Wazayuni maghasibu walilazimika kutangaza usitishaji vita baada ya jeshi la utawala wa Israel kufanya mashambulizi ya kinyama ya siku 22 dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza. Katika mashambulizi hayo, utawala wa Kizayuni ulikusudia kuiangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas au kwa uchache kuilazimisha harakati [&hellip

Jumatano, Januari 16, 2013

Jumatano, Januari 16, 2013

Siku kama hii ya leo miaka 25 iliyopita Sayyid Mahdi Hakim aliyekuwa mwanachama mashuhuri wa Majlis Kuu ya Kiislamu ya Iraq na mwana wa Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim mmoja wamarajii wakubwa wa Kiislamu aliuawa kigaidi na maajenti wa utawala wa Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq, huko Khartoum mji mkuu wa Sudan. Sayyid Mahdi [&hellip

Jumanne, 15 Januari, 2013

Jumanne, 15 Januari, 2013

Siku kama ya leo miaka 34 iliyopita Muhammad Reza Pahlavi mfalme wa mwisho wa Iran alikimbia nchi kwa kisingizio cha matibabu baada ya kupamba moto mapambano ya wananchi Waislamu wa Iran. Mwaka 1320 Hijria Shamsiya Muhammad Ridha Pahlavi alikalia kiti cha usultani baada ya serikali ya Uingereza kumbaidisha baba yake, Ridha Shah kutokana na hatua [&hellip

Jumatatu, Januari 14, 2013

Jumatatu, Januari 14, 2013

Siku kama ya leo miaka miwili iliopita, sawa na tarehe 14 Januari 2011 Rais Zainul Abidin Bin Ali wa Tunisia na dikteta wa nchi hiyo alikimbilia Saudi Arabia kufuatia vuguvugu la mapinduzi ya wananchi. Kwa kuikimbia nchi Zainul Abidin, utawala wa kiimla uliodumu kwa nusu karne wa Habib Bourquiba pamoja na Zainul Abidin Bin Ali [&hellip

Jumapili, 1 Rabiul Awwal 1434

Jumapili, 1 Rabiul Awwal 1434

Siku kama ya leo miaka 1434 iliyopita ilianza hijra ya mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Baada ya kupita kipindi cha miaka 13 cha utume wake tangu kubaathiwa mtukufu huyo, alilazimika kuhamia mjini Madina kufuatia kushadidi kwa maudhi mengi kutoka kwa washirikina wa mji wa Makka. Mtume (SAW) aliuhama mji wa Makka huku kundi moja la washirikina [&hellip