Category: Mengineyo

Jumatano, Machi 25, 2015

Jumatano, Machi 25, 2015

​Siku kama hii ya leo miaka 21 iliyopita, vikosi vya jeshi la Marekani ambavyo mwezi Disemba 1992 viliivamia Somalia kwa kisingizio cha kukomesha uasi nchini humo, hatimaye vililazimika kuondoka katika nchi hiyo baada ya kushindwa vibaya.  Mwaka 1991 makundi mbalimbali ya Somalia yalimpindua dikteta wa nchi hiyo Muhammad Siad Barre. Hata hivyo makundi hayo yalishindwa [&hellip

02 – Ayyame Fatimiyyah 1436

Jumanne, Machi 24, 2015

Jumanne, Machi 24, 2015

​Siku kama ya leo miaka 1425 iliyopita alikufa shahidi Bibi Fatima al Zahra, binti mtukufu wa Mtume wetu Muhammad (saw) na mke wa Imam Ali bin Abi Twalib (as). Alizaliwa miaka mitano baada ya kubaathiwa Nabii Muhammad (saw) na mtukufu huyo akampa jina la Fatima. Alipewa malezi na wazazi wake wawili yaani Bibi Khadija na [&hellip

Jumatatu, Machi 23, 2015

Jumatatu, Machi 23, 2015

​Siku kama ya leo miaka 10 iliyopita, sawa na tarehe 3 Farvardin 1384 Hijria Shamsia, alifariki dunia Allamah Sayyid Jalaluddin Ashtiyani, mwanafalsafa na mwanafikra wa Kiislamu baada ya kuugua kwa muda mrefu.  Allamah Ashtiyani alizaliwa mjini Ashtiyan katikati mwa Iran na kusoma masomo ya awali mjini hapo, ambapo baadaye alielekea mjini Qum na kupata elimu [&hellip

Jumamosi, Machi 21, 2015

Jumamosi, Machi 21, 2015

Leo ni tarehe Mosi Farvardin mwaka mpya wa 1394 Hijria Shamsia ambayo inasadifiana na siku ya kwanza ya mwaka wa Kiirani maarufu kwa jina la Sikukuu ya Nowruz. Nowruz ni moja kati ya sherehe za kale zaidi duniani na ilianza kusherehekewa zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Mwaka 2010 Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi Machi 21 [&hellip

Ijumaa, 20 Machi, 2015

Ijumaa, 20 Machi, 2015

Siku kama ya leo miaka 12 iliyopita sawa na tarehe 20 Machi 2003, Marekani na Uingereza kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na silaha za mauaji ya halaiki kwa pamoja ziliishambulia Iraq na kuuangusha utawala wa Saddam Hussein.  Mashambulio hayo yalipingwa na walimwengu ambao walizituhumu nchi hizo za Magharibi kwa kuchukua hatua hiyo kinyume cha [&hellip

​Alkhamisi, 19 Machi, 2015

​Alkhamisi, 19 Machi, 2015

Siku kama ya leo miaka 28 iliyopita inayosadifiana na tarehe 19 Machi 1987 alifariki dunia Louis de Broglie, ambaye alikuwa wa mwisho katika kizazi cha waasisi wa fizikia ya kisasa akiwa na umri wa miaka 95.  Louis de Broglie alizaliwa mwaka 1892 na baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia alianza utafiti wa elimu ya [&hellip

Jumatano, Machi 18, 2015

Jumatano, Machi 18, 2015

​Siku kama ya leo miaka 53 iliyopita, hatimaye mapambano ya wananchi Waislamu wa Algeria yaliyoanzishwa kwa lengo la kuikomboa nchi hiyo na kukomesha uvamizi wa kikoloni wa Ufaransa yalipata ushindi baada ya miaka minane ya vita vikali. Watu milioni moja waliuawa katika vita hivyo. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa pili wa Evian, [&hellip

Jumanne, Machi 17, 2015

Jumanne, Machi 17, 2015

Miaka 1379 iliyopita inayosadiafina na siku kama ya leo, ardhi ya Baitul Muqaddas huko Palestina ilikombolewa na Waislamu.  Vita vya kwanza kati ya Waislamu na Warumi vilijiri huko kaskazini mwa Bahari Nyekundu baada ya kudhihiri Uislamu. Jeshi la Waislamu lilitoa pigo kwa Warumi na eneo la kusini mwa Palestina likakombolewa katika zama za utawala wa [&hellip

Jumatatu, Machi 16, 2015

Jumatatu, Machi 16, 2015

Siku kama ya leo miaka 156 iliyopita kulingana na kalenda ya Miladia, Alexander Stepanovich Popov, mvumbuzi na mwanafizikia wa Russia alizaliwa.  Baada ya kuhitimu masomo yake katika taaluma ya fizikia, alianza kujishughulisha na ufundishaji katika vyuo vikuu vya nchi hiyo. Mbali na shughuli hiyo, Popov aliendelea mbele na utafiti wake katika nyanja mbalimbali za kielimu [&hellip