Category: Mengineyo

Alkhamisi, Februari 20, 2014

Alkhamisi, Februari 20, 2014

Miaka 25 iliyopita katika siku kama ya leo, inayosadifiana na tarehe Mosi Esfand 1366 Hijria Shamsia, ndege moja ya abiria ya Iran ilishambuliwa na kutunguliwa kwa kombora la majeshi ya utawala wa kidikteta wa Saddam Hussein wa Iraq na kuangushwa, wakati wa vita vya Iran na Iraq. Katika tukio hilo, Hujjatulislam Fadhlullah Mahallati, mwakilishi wa [&hellip

Jumatano, Februari 19, 2014

Jumatano, Februari 19, 2014

Siku kama ya leo miaka 541 iliyopita alizaliwa mnajimu na mwanahesabati mashuhuri wa Poland Nicolaus Copernicus. Awali alijifunza elimu ya nujumu na baadaye tiba, na baada ya kukamilisha masomo alianza kufundisha hesabati huko Roma. Hata hivyo Copernicus aliendelea kudurusu na kufanya utafiti wa elimu ya nujumu na mwaka 1503 alivumbua nadharia ya harakati ya dunia [&hellip

Jumanne, Februari 18, 2014

Jumanne, Februari 18, 2014

Siku kama ya leo miaka 49 iliyopita nchi ya Gambia ilifanikiwa kupata uhuru kutoka kwa mkoloni Mwingereza na siku kama ya leo hujulikana nchini humo kama siku ya kitaifa. Gambia ilikuwa koloni la kwanza la Uingereza barani Afrika. Uingereza iliikoloni nchi hiyo tangu mwaka 1588 na kuendelea kupora maliasili ya nchi hiyo kwa karibu karne [&hellip

Faida na Madhara ya Chumvi

Faida na Madhara ya Chumvi

Ahlan wa sahlan wasikilizaji wapenzi na karibuni kujumuika nami katika kipindi hiki cha Ijuwe Afya Yako ambapo juma hili kitazungumzia faida na madhara ya chumvi. Tangu enzi na enzi, chumvi imekuwa miongoni mwa viungo muhimu vya chakula. Mbali na kuwa na madhara inapotumiwa vibaya, lakini bado ni muhimu kwa mwili wa binadamu. Chumvi ni aina [&hellip

Jumamosi, Februari 15, 2014

Jumamosi, Februari 15, 2014

Siku kama ya leo miaka 25 iliyopita, jeshi Jekundu la Shirikisho la Urusi ya Zamani lililazimika kuondoka nchini Afghanistan baada ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo kwa miaka kumi. Majeshi hayo yaliondoka baada ya kushindwa kukabiliana na muqawama wa mujahidina wa Kiislamu. Lengo la Umoja wa Sovieti la kuivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan mwaka [&hellip

Ijumaa, 14 Februari, 2014

Ijumaa, 14 Februari, 2014

Siku kama hii ya leo miaka 25 iliyopita sawa na tarehe 25 Bahman mwaka 1367 Hijria Shamsia mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Ruhullah Khomeini alitoa fatuwa ya hukumu ya kifo dhidi Salman Rushdie, mwandishi wa kitabu cha ‘Aya za Kishetani’ baada ya kumtangaza kuwa ameritadi. Katika kitabu hicho Rushdie alimvunjia heshima na [&hellip

Alkhamisi, Februari 13, 2014

Alkhamisi, Februari 13, 2014

Siku kama ya leo miaka 1217 iliyopita alifariki dunia mwanahistoria mkubwa wa Kiarabu Abu Muhammad Abdul-Malik Bin Hisham, maarufu kwa jina la “Ibn Hisham.” Ibn Hisham alizaliwa mjini Basra kusini mwa Iraq ya leo na kutumia umri wake mwingi katika utafiti kuhusiana na maisha ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Alikuwa mtaalamu mashuhuri duniani katika lugha [&hellip

Jumatano, Februari 12, 2014

Jumatano, Februari 12, 2014

Siku kama ya leo miaka 205 iliyopita alizaliwa mtaalamu wa sayansi asilia wa Uingereza Charles Darwin. Msomi huyo alifanya utafiti kuhusu namna ya kutokea viumbe mbalimbali na alifanya safari ya muda mrefu duniani kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi wake wa kielimu. Baada tu ya kurejea aliandika kitabu maarufu cha “On the Origin of Species”. Kwa [&hellip

Jumanne, Februari 11, 2014

Jumanne, Februari 11, 2014

Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita Iran ilishuhudia moja ya siku za kihistoria. Siku hiyo Iran ilifungua ukurasa mpya kwa sauti za Allah Akbar, kujitolea kwa wananchi na uongozi wa hayati Imam Khomeini. Siku hiyo Iran iliondoka katika giza la utawala wa Kifalme na kutangaza Jamhuri ya Kiislamu. Wananchi wa matabaka na rika zote, [&hellip

Jumatatu, 10 Februari, 2014

Jumatatu, 10 Februari, 2014

Siku kama ya leo miaka 1234 iliyopita inayosadifiana na tarehe 10 Rabiu Thani  mwaka 201 Hijria, alifariki dunia Bibi Fatima Maasuma A.S, binti wa Imam Mussa bin Jaafar A.S mmoja wa wajukuu watukufu wa Bwana Mtume Muhammad SAW. Bibi Fatima Maasuma alizaliwa mwaka 173 Hijria katika mji wa Madina. Alikuwa mwanamke mwenye fasaha, alimu, hodari [&hellip