Category: Mengineyo

Jumatano, Novemba 26, 2014

Jumatano, Novemba 26, 2014

Siku kama ya leo miaka 1379 iliyopita, kwa mujibu wa baadhi ya nukuu za historia alizaliwa Imam Muhammad Baqir AS mjukuu mtukufu wa Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW) na mmoja wa Maimamu watoharifu katika kizazi chake. Imam Baqir AS alizaliwa katika mji mtakatifu wa Madina na alikuwa mashuhuri kwa elimu kubwa na maarifa, ambapo alikuwa [&hellip

Jumanne, 25 Novemba, 2014

Jumanne, 25 Novemba, 2014

Siku kama ya leo miaka 1315 iliyopita aliuawa shahidi Zaid bin Ali bin Hussein mwana wa Imam Sajjad (as) na mjukuu wa Mtume Muhammad (saw). Zaid bin Ali alisimama kupambana na dhulma za Banii Umayyah na kulinda matunda ya mapambano ya babu yake, Imam Hussein bin Ali (as). Baada ya mapambano ya kishujaa, Zaid bin [&hellip

Jumatatu, Novemba 24, 2014

Jumatatu, Novemba 24, 2014

Siku kama ya leo miaka 1399 iliyopita, awamu ya mwisho ya vita kati ya jeshi la Imam Ali bin Abi Twalib (as) na Muawiya bin Abi Sufian ilianza katika eneo la Siffin kandokando ya Mto Furati (Euphrates) nchini Iraq. Baada ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) kushika hatamu za uongozi Muawiya alikataa kumpa mkono [&hellip

Jumamosi, Novemba 22, 2014

Jumamosi, Novemba 22, 2014

Siku kama ya leo miaka 47 iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 242 kuhusu Palestina. Miongoni mwa vipengee vya azimio hilo ni udharura wa kuondoka askari wa utawala ghasibu wa Israel katika ardhi zote za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu Juni mwaka 1967 katika vita vya Waarabu na Israel, kusimamishwa operesheni [&hellip

Alkhamisi, 20 Novemba, 2014

Alkhamisi, 20 Novemba, 2014

Siku kama ya leo miaka 104 iliyopita alifariki dunia mwandishi mashuhuri wa Kirusi Leo Tolstoy. Mwandishi huyo alizaliwa mwaka 1828 na aliondokewa na baba na mama yake akiwa bado mdogo. Alifanya safari za kitalii na uchunguzi katika jamii nyingi za Ulaya na mambo aliyoyashuhudia katika safari hizo yalimfanya achukie ustaarabu wa kimaada wa nchi za [&hellip

Jumatano, Novemba 19, 2014

Jumatano, Novemba 19, 2014

Siku kama ya leo miaka 1341 inayosadifiana na tarehe 25 Muharram mwaka 95 Hijria, kwa mujibu wa baadhi ya nukuu za historia, aliuawa shahidi Ali bin Hussein mwenye lakabu ya Sajjad na Zainul Abidiin AS, mtoto wa Imam Hussein bin Ali AS, na mjukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad SAW. Imam Zainul Abidiin AS alizaliwa mjini [&hellip

Jumanne, Novemba 18, 2014

Jumanne, Novemba 18, 2014

Siku kama ya leo miaka 175 iliyopita ilianza awamu ya pili ya mapambano ya wananchi wa Algeria wakiongozwa na Abdul Qadir bin Muhyiddin dhidi ya ukoloni wa Ufaransa. Ufaransa iliivamia Algeria mwaka 1830 ikiwa na nia ya kuikalia kwa mabavu nchi hiyo. Amir Abdul Qadir akiwa pamoja na wapiganaji elfu 50 alipambana na wakoloni wa [&hellip

Jumatatu, Novemba 17, 2014

Jumatatu, Novemba 17, 2014

Siku kama ya leo miaka 145 iliyopita, mfereji wa Suez ambao unauinganisha bahari ya Mediterranian na Bahari Nyekundu ulifunguliwa. Mfereji huo wenye urefu wa kilometa 167 na upana wa mita 120 hadi 200 ulichimbwa chini ya usimamizi wa mhandisi wa Ufaransa, Ferdinand de Lesseps. Mfereji wa Suez pia unahesabiwa kuwa mpaka kati ya bara la [&hellip

Uislamu na Mtindo wa Maisha (5)

Uislamu na Mtindo wa Maisha (5)

Hamjambo wasikilizaji wapenzi na karibuni kuwa nami tena katika sehemu nyingine ya kipindi cha Uislamu na Mtindo wa Maisha. Kipindi chetu cha wiki hii kitakamilisha sehemu iliyopita na kutazama itikadi zenye taathira katika mtindo wa maisha katika aidiolojia ya Kiislamu. Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kuwa kando ya redio zenu kusikiliza niliyokuandalieni. Miongoni mwa sababu [&hellip

Jumamosi, Novemba 15, 2014

Jumamosi, Novemba 15, 2014

Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita, alifariki dunia Allamah Muhammad Hussein Tabatabai akiwa na umri wa miaka 80. Mwanazuoni huyo mkubwa alizaliwa katika mji wa Tabriz, kaskazini magharibi mwa Iran. Msomi huyo mkubwa wa Kiislamu alikuwa hodari sana katika elimu za falsafa, irfani, tafsiri ya Qur’ani na vilevile katika masuala ya fasihi, hisabati na [&hellip