Category: Habari za Kimataifa
Zuma kuelekea Zimbabwe ili kuziba ufa katika serikali ya muungano
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini anatarajiwa kuelekea nchini Zimbabwe wakati wowote kutoka sasa ili kutatua mifarakano inayoendelea kujitokeza kati ya viongozi wakuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo. Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC siku ya Ijumaa walimtaka Rais Zuma kufunga safari mara moja na kuelekea Harare
Serikali ya Syria yawatimua mabalozi wa nchi kadhaa za Ulaya nchini humo
Serikali ya Syria imewatimua mabalozi wa nchi kadhaa za Ulaya nchini humo kutokana na kile ilichokiita kuwa ni mabalozi hao kufanya mambo yasiyofaa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetangaza kuwa, mabalozi kadhaa wa nchi za Ulaya hawafai kuendelea kubakia nchini humo kutokana na mwenendo wao mbaya. Serikali ya Damascus imewafukuza mabalozi hao kwa
Wilayati: Kundi la 5+1 linapaswa kutambua rasmi haki za nyuklia za Iran
Mshauri wa masuala ya kimataifa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema ili yaweze kupatikana mafanikio katika mazungumzo ya Moscow, kundi la 5+1 linapaswa kutambua rasmi haki za nyuklia za Iran. Ali Akbar Wilayati amesisitiza kuwa ikiwa kundi la 5+1 linataka mazungumzo yajayo yatakayofanyika katika mji mkuu wa Russai, Moscow yawe mazungumzo ya maana
Jumanne, Juni 5, 2012
Leo ni Jumanne tarehe 14 Rajab mwaka 1433 Hijria inayosadiafina na tarehe 5 Juni 2012 Miladia. Siku kama ya leo miaka 23 iliyopita sawa na tarehe 16 Khordad 1368 Hijria Shamsia, mamilioni ya wananchi wa Iran waliojawa na huzuni kubwa waliuzika mwili wa Imam Khomeini MA karibu na makaburi ya mashahidi wa vita vya kulazimishwa
Kuendelea jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya mateka wa Kipalestina na ahadi hewa za Umoja wa Mataifa
Kuendelea jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya mateka wa Kipalestina wanaozuiliwa katika jela za kuogofya za utawala huo kunaendelea kukabiliwa na radiamali tofauti kutoka ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo na vilevile katika ngazi za kimataifa. Katika upande wa ndani, Issa Qaraqe’ Waziri wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina anayeshughulikia Masuala ya
Ufaransa yatahadharisha uwezekano wa kujitoa Ugiriki katika eneo la Euro
Waziri wa Fedha wa Ufaransa amesema kuwa, iwapo baada ya uchaguzi Ugiriki itaendelea kutoheshimu makubaliano ya kuinasua nchi hiyo katika mgogoro wa kifedha, kuna uwezekano wa nchi hiyo kujitoa katika muungano wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro. Pierre Moscovici amesema, iwapo Ugiriki itashindwa kuheshimu makubaliano hayo, nchi za Ulaya zitajikuta katika hali ngumu na kuitaka
Kundi la Watu wenye silaha lauzingira uwanja wa ndege wa Tripoli nchini Libya
Habari kutoka Tripoli, mji mkuu wa Libya zinasema kuwa watu wenye silaha wameuzingira uwanja wa ndege wa kimataifa mjini humo na hivyo kulazimu ndege kutua katika uwanja mdogo wa ndege wa kijeshi viungani mwa mji mkuu huo. Watu hao wanadaiwa kutoka katika mji wa Tarhouna ulioko kilomita 80 kusini mashariki mwa Tripoli. Habari zaidi zinasema
Watu 33 wameuawa na wengine 100 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu nchini Iraq
Idadi ya watu waliouawa katika mlipuko wa bomu huko Baghdad imeongezeka na kufikia 32. Mlipuko huo umetokea leo mchana karibu na ofisi za iadara ya Waqfu wa Mashia katika eneo la Babul Muadham lililoko mjini Baghdad na kuwaua watu 32 sambamba na kuwajeruhi wengine wapatao 100. Katika tukio hilo la kigaidi nyumba kadhaa za idara
Chama cha Annahdha chataka kufanyike mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa Tunisia
Mkuu wa chama cha Kiislamu cha Annahdha nchini Tunisia ametoa wito wa kufanyika mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa ili kuondoa wingu la uhasama linaloendelea kufunika anga ya kisiasa na kijamii nchini humo. Rashid Ghanouchi amesema kuwa malengo ya mapinduzi hayawezi kufikiwa katika anga ya mfarakano na chuki na ametaka makundi yote yanayojaribu kuwatenganisha wananchi yakome
Ikhwanul Muslimina: Muhammad Morsi hatasalimu amri mbele ya Marekani
Naibu kiongozi wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la kisiasa la Harakati ya Ikhwanul muslimina nchini Misri amesema kuwa, Muhammad Morsi, ambaye ni mgombea wa kiti cha rais wa Misri kwa tiketi ya chama hicho kamwe hatasalimu amri mbele ya vitisho vya Marekani na washirika wake. Isam al Uryan ameyasema hayo hii leo na





