Category: Michezo

Diego Simeone ajifunga Atletico Madrid mpaka 2020.

Diego Simeone ajifunga Atletico Madrid mpaka 2020.

Kocha wa Klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amezima tetesi za kuhamia klabu ya Inter Milan ya Italia baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kufundisha miamba hiyo ya jiji la Madrid. Mu argentina huyo alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa vigogo hao wa Italia, ambao aliwachezea kuanzia mwaka 1997 hadi 1999, lakini ameamua [&hellip

Msuva Aleta Shangwe Stars.

Msuva Aleta Shangwe Stars.

Mchezaji wa kimataifa, Simon Msuva jana alionesha matunda yake ya kucheza soka ya kulipwa katika timu ya Difaa Hassan El-Jadida ya Morocco baada ya kuifungia Taifa Stars mabao dhidi ya Botswana. Katika mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Msuva alikuwa mwiba mchungu kwa Botswana na mabao yake [&hellip

Ubelgiji Yafuzu Kwa Kombe La Dunia.

Ubelgiji Yafuzu Kwa Kombe La Dunia.

Ubelgiji imekuwa taifa la kwanza kutoka Ulaya kujiunga na wenyeji Urusi katika kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi dhidi ya Ugiriki wa 2-1 kupitia mabao kutoka kwa Jan Vertonghen na Romelu Lukaku. Magoli yote matatu yalifungwa katika dakika tano kipindi cha pili, Vertonghen akitangulia kwa kuiweka Ubelgiji kifua mbele. José [&hellip

Ufaransa yashindwa kuilaza Luxembourg ikiwa na Pogba, Griezmann, Mbappe na Lemar.

Ufaransa yashindwa kuilaza Luxembourg ikiwa na Pogba, Griezmann, Mbappe na Lemar.

Mkufunzi wa timu ya taifa Ufaransa Didier Deschamps ameachwa akiwa na ”ghadhabu” baada ya timu yake kushindwa kuifunga Luxembourg licha ya kupata nafasi nyingi, matokeo yaliyotajwa kuwa ya ”kihistoria” na mwenzake wa Luxembourg. Mechi hiyo iliyochezwa Ufaransa ilimalizika kwa sare tasa. Ufaransa ilimiliki mpira katika mchezo huo kwa asilimia 76, na kushambulia mara 34 na [&hellip

Arsene Wenger asema ‘alisita’ kutia saini mkataba mpya Arsenal.

Arsene Wenger asema ‘alisita’ kutia saini mkataba mpya Arsenal.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ”alisita” wakati wa kutia saini mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita kwa sababu hakuwa na uhakika kwamba ”angeweza kuiongoza klabu hiyo.” Wenger alikubali mkataba wa miaka miwili mwezi Mei, mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika. Kwenye runinga moja nchini Ufaransa ya Telefoot, alisema alikuwa na ”sababu za kibinafsi” [&hellip

La Liga Yaishitaki Man City, Matumizi Makubwa Ya Fedha.

La Liga Yaishitaki Man City, Matumizi Makubwa Ya Fedha.

Shirikisho la soka nchini Hispania (La Liga) limeliandikia barua shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) wakitoa malalamiko kuhusu ukiukwaji wa sheria za matumizi Financia Fair Play (FFP) unaofanywa na klabu ya Man City. Raisi wa La Liga Javier Tebas alitoa malalamiko kuhusu wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia ni wamiliki wa klabu ya [&hellip

Oxlade Chamberlain aikataa Chelsea, ataka kwenda Liverpool.

Oxlade Chamberlain aikataa Chelsea, ataka kwenda Liverpool.

Kiungo wa kati wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain amekataa uhamisho wa Chelsea baada ya klabu hiyo kukubali dau la £40m. Oxlade Chamberlain anaamini kwamba Chelsea ilipanga kumtumia kama beki wa kulia huku lengo lake kuu la kutaka kutoka Arsenal likiwa hatua ya kuchezeshwa katikati. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa anataka kuelekea Liverpool. [&hellip

Souare arejea dimbani baada ya Mwaka.

Souare arejea dimbani baada ya Mwaka.

Beki wa Crystal Palace Pape Souare amerejea uwanjan toka alipopata ajali mbaya ya gari na kusababisha kuvunjika mfupa wa nyonga na taya. Souare mwenye umri wa miaka 27 alipata ajali ya gari mwezi Septemba mwaka 2016 na alirejea mazoezi na klabu yake mwanzoni mwa mwezi huu. Mlinzi huyo wa kulia raia wa Senegal alicheza kwa [&hellip

Wenger awataka mashabiki kudumisha imani baada ya kichapo Anfield.

Wenger awataka mashabiki kudumisha imani baada ya kichapo Anfield.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuwa na imani baada ya kile alichosema kuwa ni uchezaji wa kusikitisha sana baada ya klabu hiyo kucharazwa na Liverpool 4-0 katika mechi ya Ligi ya Premia Jumapili. Gunners hawakuwa na kombora hata moja lililolenga goli baada ya uchezaji mbaya ambao ulikosolewa pakubwa na [&hellip

Lipuli yaiduwaza Yanga.

Lipuli yaiduwaza Yanga.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara, Yanga jana iliduwazwa na Lipuli kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mechi yake ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Matokeo hayo hayakutarajiwa na wengi kutokana na ugeni wa Lipuli kwenye ligi na hivyo iliingia uwanjani ikiwa haipewi nafasi ya kushinda. Lipuli iliyopanda Ligi Kuu [&hellip