Category: Habari za Kitaifa

Sakata la Wizi wa Makontena Watuhumiwa 12 Washikiliwa na Jeshi la Polisi.

Sakata la Wizi wa Makontena Watuhumiwa 12 Washikiliwa na Jeshi la Polisi.

    Jeshi la Polisi nchini limesema zaidi ya watuhumiwa 12 wamekamatwa kufuatia uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika uchunguzi wa makosa ya uhalifu wa kifedha wa jeshi hilo, kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa dhidi ya wahusika wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam   Akizungumza na Waandishi wa [&hellip

Shehe Ponda Aachiwa Huru.

Shehe Ponda Aachiwa Huru.

    Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda ameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro baada ya kumwona hana hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili. Shehe Ponda alifunguliwa kesi namba 128, Agosti 19, 2013 katika mahakama hiyo baada ya kudaiwa kutenda kosa la kuvunja sheria ya [&hellip

Pesa za Sherehe ya Uhuru Kujenga Barabara.

Pesa za Sherehe ya Uhuru Kujenga Barabara.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za [&hellip

Watakaoshindwa Kupeleka Watoto Shuleni Kukiona.

Watakaoshindwa Kupeleka Watoto Shuleni Kukiona.

    Serikali  imeonya kuwa itawachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi watakaoshindwa kuwapeleka watoto shule na kusisitiza kila mtoto anapaswa kupewa haki ya kupata elimu itakayoanza kutolewa bure kuanzia Januari.   Sera ya utoaji wa elimu bure ni moja ya vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ili [&hellip

Bakhresa Achunguzwa.

Bakhresa Achunguzwa.

      Kampuni  ya Said Salim Bakhresa (SSB) inachunguzwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kushiriki kukwepa kodi na hivyo kuikosesha serikali mabilioni ya fedha kutokana na makontena yaliyohifadhiwa kwenye bandari yake ya nchi kavu (ICD) ‘kupotea’ bila kulipiwa kodi. Tayari Mamlaka ya Mapato (TRA) imepiga marufuku SSB kuingiza makontena katika bandari hiyo [&hellip

MSD Kuzindua Duka la Dawa MNH J’tatu.

MSD Kuzindua Duka la Dawa MNH J’tatu.

  Bohari  ya Dawa (MSD), imeanza mikakati ya kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kufungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambalo litazinduliwa rasmi Jumatatu.   Imesema mbali na duka hilo, wako mbioni kufungua maduka mengine ya dawa kwenye hospitali zote za wilaya na mikoa hapa nchini ili kusogeza huduma [&hellip

Milioni 300/- Zaokolewa, Kukamatwa Kwa Kontena 37.

Milioni 300/- Zaokolewa, Kukamatwa Kwa Kontena 37.

    Kontena 37 zenye shehena ya magogo aina ya mninga yenye thamani zaidi ya Sh. milioni 300 zimekamatwa zikiwa zinasafirishwa kuelekea nchini China bila kibali.   Katika shehena hiyo, kontena 31 zimekamatiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kati ya hizo mbili zimekamatwa mkoani Mbeya,  na mikoa ya Rukwa na Pwani katika maeneo ya [&hellip

Makubaliano CUF, CCM Bado.

Makubaliano CUF, CCM Bado.

    Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema mazungumzo yanayoshirikisha viongozi wa vyama viwili vya siasa vya CCM na CUF, yanaendelea na hakuna makubaliano yaliyofikiwa hadi sasa ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu uliofutwa wa Oktoba 25.   Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa ufafanuzi kuhusu [&hellip

Mtikisiko Vigogo TRA.

Mtikisiko Vigogo TRA.

    Rais  John Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, muda mfupi baada ya ziara ya kushitukiza ya Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa iliyofanyika jana.   Taarifa ya jana ya Ikulu iliyomnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imeeleza kuwa hatua hiyo ya Dk Magufuli imechukuliwa baada ya [&hellip

Zoezi La Usafi Kuwa Endelevu Jijini Dar es salaam.

Zoezi La Usafi Kuwa Endelevu Jijini Dar es salaam.

    Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Mhe. Said Meck Sadiki amesema zoezi la usafi wa mazingira litakalofanyika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, litakuwa ni endelevu kwa mkoa wa Dar es Salaam hata baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo. Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa [&hellip