Category: Habari

Tetemeko Baya Lakumba Taiwan.

Tetemeko Baya Lakumba Taiwan.

  Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki. Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan. Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali [&hellip

Jaji wa Mahakama ya Kilele Kenya Apatikana na Hatia ya Kula Rushwa.

Jaji wa Mahakama ya Kilele Kenya Apatikana na Hatia ya Kula Rushwa.

    Kamisheni inayohusika na huduma za mahakama nchini Kenya (JSC) imependekeza kuundwa jopo maalumu la kuchunguza zaidi tuhuma za ufisadi dhidi ya jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini humo, Philip Tunoi. Jaji Mkuu wa Kenya, Willie Mutunga amesema ripoti za awali zinaonyesha kuwa, Jaji Tunoi alihusika kwenye kashfa ya kupokea hongo na kwa [&hellip

Burundi Yatuhumiwa Kuwaandama Wapinzani Tanzania.

Burundi Yatuhumiwa Kuwaandama Wapinzani Tanzania.

    Wakimbizi kutoka Burundi ambao wametorokea katika nchi jirani ya Tanzania wameituhumu serikali ya Bujumbura kuwa inatuma watu waliojizatiti kwa silaha kwenda kukabiliana na wafuasi wa upinzani miongoni mwao katika kambi za wakimbizi za Tanzania. Kanali ya Televisheni ya Al-Jazeera imeripoti kuwa, wakimbizi raia wa Burundi wamesema kuwa maisha yao yamo hatarini katika kambi [&hellip

Canada Yaiondolea Vikwazo Iran, Kufungua Ubalozi.

Canada Yaiondolea Vikwazo Iran, Kufungua Ubalozi.

    Canada imesema kuwa imeiondolea Iran baadhi ya vikwazo na kwamba inaandaa mazingira ya kuhuisha uhusiano wake wa kidiplomasia na Jamhuri ya Kiislamu. Serikali ya Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada imeyasema hayo jana Ijumaa na kuongeza kuwa, imeangalia upya uhusiano wake na nchi hii na kwamba sasa itayaruhusu tena makampuni ya nchi hiyo [&hellip

Al-Shabab Wadhibiti Bandari ya Marka, Somalia.

Al-Shabab Wadhibiti Bandari ya Marka, Somalia.

    Habari kutoka Somalia zinasema kuwa, magaidi wa al-Shabab wamechukua udhibiti wa bandari muhimu na ya kistratejia ya Marka baada ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AMISOM) kuondoka katika eneo hilo. Ibrahim Adam, afisa mwandamizi wa usalama katika eneo la Lower Shebelle amesema wanajeshi wa Uganda ambao ni sehemu ya AMISOM [&hellip

Kaburi La Umati La Waislamu Wa Zaria Lagunduliwa.

Kaburi La Umati La Waislamu Wa Zaria Lagunduliwa.

      Wanaharakati wa Nigeria wamegundua kaburi la umati la Waislamu waliouawa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria. Ripoti zinasema kuwa wanaharakati wa Nigeria wametangaza kuwa kaburi hilo lililogunduliwa katika makaburi ya Mando Kaduna ni moja ya makaburi ya umati ambamo jeshi la Nigeria lilizika zaidi ya maiti za Waislamu 1000 [&hellip

Mramba na Yona Kutumikia Kifungo Cha Nje.

Mramba na Yona Kutumikia Kifungo Cha Nje.

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.   Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili [&hellip

Imani za Kishirikina Zinaua Albino.

Imani za Kishirikina Zinaua Albino.

    Watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) kati ya 40 hadi 43 wameuawa na watu wasiojulikana katika kipindi kati ya mwaka 2006 na 2014 kutokana na imani mbalimbali ikiwemo ushirikina.   Hayo yamo katika majibu aliyotoa bungeni jana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni alipokuwa akijibu swali nyongeza la Mbunge wa [&hellip

Walio Mdhalilisha Mtanzania Wakamatwa India.

Walio Mdhalilisha Mtanzania Wakamatwa India.

  Waziri wa mambo ya nje ya nchi, ushirikiano wa kimataifa na kikanda Africa Mashariki Balozi Dr. Augustine Mahiga ametoa kauli bungeni kuhususiana na sakata la kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa  kitanzania anaesoma  nchini India ambapo amesema tayari waliofanya  hivyo wamefikishwa mahakani. Balozi Mahiga amesema jana walimuita balozi wa India aliyopo hapa  nchini na kuzungumzia swala [&hellip

Zitto Atoswa na Kambi Rasmi ya Upinzani.

Zitto Atoswa na Kambi Rasmi ya Upinzani.

    Kambi rasmi ya upinzani bungeni, imetangaza baraza lake la mawaziri kivuli ambalo Chama cha ACT Wazalendo, chenye mbunge mmoja, Kabwe Zitto, ndicho hakikuingizwa kwenye baraza hilo. Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alitangaza jana bungeni baraza hilo.   Chadema chenye wabunge wengi katika kambi hiyo, kina mawaziri vivuli wengi ikilinganishwa na vyama vingine [&hellip