Articles By: admin

Rubani wa Urusi Aokolewa Syria.

Rubani wa Urusi Aokolewa Syria.

    Urusi inasema kuwa msaidizi wa rubani wa ndege ya kijeshi iliyodunguliwa na Uturuki hapo jana ameokolewa na kurejeshwa katika kambi yao ya kijeshi iliyoo Syria. Urusi inasema kuwa afisa huyo yuko katika hali njema katika kambi ya kijeshi ya Lattakia. Wizara ya ulinzi nchini Urusi inasema kuwa rubani mwingine na mwanajeshi aliyeshiriki katika [&hellip

Mvulana Aliyetuhumiwa Kuwa ‘Gaidi’ Adai Fidia.

Mvulana Aliyetuhumiwa Kuwa ‘Gaidi’ Adai Fidia.

    Mvulana wa umri wa miaka 14 aliyezoa umaarufu baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, anadai fidia ya dola milioni 15 ($15m). Ahmed Mohammed alitiwa mbaroni na polisi wa mji wa Irving, jimbo la Texas nchini Marekani baada ya saa yake kudhaniwa kuwa kilipuzi na baadaye akafukuzwa shule. Taarifa ya wakili [&hellip

Muongozo Elimu Bure Waandaliwa.

Muongozo Elimu Bure Waandaliwa.

    Katibu  Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, amesema wizara yake inaandaa mwongozo utakaotoa maelekezo juu ya muundo, mfumo na utaratibu nyumbufu utakaohakikisha kuwa ifikapo Januari mwakani, elimu ya msingi inatolewa bila malipo.   Profesa Mchome aliyasema hayo juzi jioni katika kikao na watendaji wakuu wa taasisi zote [&hellip

Ndege Mbili Vita Dhidi ya Ujangili.

Ndege Mbili Vita Dhidi ya Ujangili.

    Serikali ya Ujerumani imeipatia Tanzania msaada wa ndege mbili za doria kwa ajili ya kukabiliana na ujangili wawanyamapori wakiwemo tembo katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba. Akizungumza jijini Arusha mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) bw. Alan Kijazi amesema ndege hizo zenye thamani ya dola laki tano zinatarajiwa kuwasili nchini [&hellip

Ayatullah Khamenei: Siasa za Marekani Zipigwe Vita.

Ayatullah Khamenei: Siasa za Marekani Zipigwe Vita.

    Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuna udharura kukabiliana na siasa za Marekani za kutaka kubadili utambulisho wa mataifa mengine kupitia njia ya kuimarisha azma na kuzidisha ushirikiano. Ayatullahil-Udhma Sayyid Ali Khamenei, ameyasema hayo mjini Tehran katika mazungumzo yake na Rais Evo Morales wa Bolivia. Amepongeza kusimama imara na kishujaa kwa Bolivia [&hellip

Burundi Yaendelea Kushuhudia Machafuko na Mauaji.

Burundi Yaendelea Kushuhudia Machafuko na Mauaji.

    Burundi imeendelea kushuhudia machafuko baada ya watu wawili kuripotiwa kuuawa leo mashariki mwa nchi hiyo. Vyombo vya usalama vinaripoti kwamba, polisi na raia mmoja wameuawa leo kufuatia shambulio dhidi ya hoteli moja katika eneo la Gisuru mashariki mwa Burundi. Tangu kuanza machafuko nchini Burundi Aprili mwaka huu, hii ni mara ya kwanza eneo [&hellip

Uhuru hapa ni kazi tu.

Uhuru hapa ni kazi tu.

    RAIS John Magufuli amewataka Watanzania popote walipo kusherehekea siku ya Uhuru, Desemba 9, 2015, kwa kufanya kazi. Taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam jana, ilisema kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) nchini.   “Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote [&hellip

Uturuki ‘Yadungua Ndege ya Urusi Syria’.

Uturuki ‘Yadungua Ndege ya Urusi Syria’.

      Ndege za kijeshi za Uturuki zimeripotiwa kudungua ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wake na Syria. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema ndege aina ya Su-24 ilianguka katika ardhi ya Syria baada ya ksuahmbuliwa kutoka ardhini, na kwamba marubani walifanikiwa kutoka kabla ya ndege hiyo kushika moto na kuanguka. Lakini [&hellip

Picha za Washukiwa wa Milipuko ya Mali Zasambazwa.

Picha za Washukiwa wa Milipuko ya Mali Zasambazwa.

    Maafisa nchini Mali leo wameonyesha picha za mwanaume na mwanamke waliowataja kuwa walisaidia mpango wa kuishambulia hoteli ya Radisson Blu huko Bamako, ambapo watu 19 na wafanya mashambulizi wawili waliuawa. Kwa mara ya kwanza maafisa wa Mali wamesema kuwa walikuwa wanawasaka watu waliohusika na shambulio hilo la kigaidi katika hoteli ya Radisson Blue [&hellip

Ubelgiji bado iko katika hali ya tahadhari

Ubelgiji bado iko katika hali ya tahadhari

Ubelgiji imeendelea kubakia katika kiwango cha juu cha hali ya tahadhari kwa siku ya tatu mfululizo, huku mfumo wa matreni ya chini ya ardhi ukiendelea kufungwa na shule pamoja na vyuo vikuu pia vikifungwa.  Polisi wanawajohi watu 21 inayowashikilia kutokana na operesheni za kupambana na ugaidi. Watu 16 walikamatwa jana jioni wakati wa operesheni kubwa [&hellip