Saudi Arabia yaua raia 79 Yemen masaa 48 yaliyopita.


Smokes rises from near the Yemeni Government TV building, background, during clashes between Sunni militiamen and Hawthi Shiite rebels in Sanaa, Yemen, Saturday, Sept. 20, 2014. The Hawthi fighters and militias and army units allied with the Muslim Brotherhood’s Islah party battled in Sanaa for a third day Saturday in clashes that have shaken the Yemeni capital, killed over 120 people, and led to thousands fleeing their homes. The violence raises fears that this chronically unstable country could be dragged into the sort of sectarian conflicts that have plagued other nations in the region. (AP Photo/Hani Mohammed)

Duru za usalama na hospitali nchini Yemen zimeripoti kuwa ndege za kivita za Saudi Arabia zimeua raia wasiopungua 79 katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita katika mkoa wa al Hudaydah pekee.
Mauaji hayo yamefanyika katika mfululizo wa mashambulizi ya anga yanayoendelea kufanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia ikisaidiwa na Marekani na Imarati dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen.
Mauaji hayo ya raia wasio na hatia wa Yemen yamejibiwa na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah ambao wamevurumisha maroketi ya Katyusha dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na vibaraka wa Saudi Arabia huko Mahall al Majarah na kandokando ya eneo al Alab.
Jeshi la Yemen na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah pia wamewashambulia mamluki wa Saudi Arabia na washirika wake katika eneo la Ajashir huko Najran na kuua kadhaa miongoni mwao.
Makumi ya mamluki wengine wa Saudia wameuawa katika operesheni ya jeshi la Yemen katika pwani ya magharibi na mkoani Taez. Vilevile gari la askari wa Saudi Arabia limeshambuliwa katika eneo la Thamirul Jamal katika mkoa wa Jizan na wanasheji wote waliokuwemo wameangamizwa.

Leave a Comment