Watu 50 Wafariki Kwa Ajali Ya Basi Nchini Kenya.


Watu 50 wamefariki dunia leo, Oktoba 10, 2018, na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya ajali ya basi la abiria lililokuwa likitokea Nairobi kuelekea Kisumu kuacha njia na kupinduka katika eneo la Fort Tenan, barabara ya Londiani-Muhoroni, Kaunti ya Kericho, Kenya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kericho, James Mogera, basi hilo lilikuwa na watu 67 na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kugonga nguzo ya reli ambapo lilipoteza mwelekeo na kupinduka umbali wa mita takribani 20 kutoka barabarani.
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Zahanati ya Fort Ternan na Hospitali ya Muhoroni kwa matibabu. Kati ya yao waliofariki, tisa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Leave a Comment