Mourinho kwa Pogba: hakuna mchezaji mkubwa kuliko Man United.


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amethibitisha kuwa kiungo wake Paul Pogba atacheza kwenye mchezo wa kesho dhidi ya West ham ingawa amesisitiza hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu.
Hii inakuja baada ya picha fupi ya video kusambaa siku ya Jumatano ikiwaonyesha wawili hao wasioiva katika chungu kimoja wakikwaruzana.
Mourinho amesema ana mahusiano mazuri na Pogba,25, pamoja na kuwa alimwambia hataendelea na unahodha tena katika timu ya Manchester United.
‘Kesho atacheza, ni mchezaji kama wachezaji wengine’.
“Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu’. Ninafuraha anavyofanya kazi yake, kama nisingefurahia asingecheza, nimefurahishwa zaidi na mazoezi yake wiki hili, amefanya mazoezi kweli, timu inahitaji mchezaji mzuri na Pogba ni mchezaji mzuri.” amesema

Akizungumza kama mgogoro wa katikati ya wiki utaleta athari yoyote amesema Manchester United ni kubwa kuliko yeyote hapa, lazima ni tetee hilo.
Hii inakuja baada ya Mourinho kumwambia Pogba hataendelea kuwa nahodha tena.
“Nilimwambia Pogba, Wachezaji na Viongozi wezangu sababu ya kwanini hataendelea kuwa Kapteni msaidizi, hivyo wote wanajua sababu ya kumuondoa Pogba kuwa nahodha wa timu.

Leave a Comment