Yanga imemuaga Canavaro.


Klabu ya Yanga iliandaa mchezo wa majaribio dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza Mawezi maalumu kwa ajili ya kumuaga mchezaji wao Nadir Haroub ‘Canavaro’.
Canavaro aliyeitumikia Yanga zaidi ya miaka 10, amestaafishwa msimu huu na kupewa nafasi ya Meneja kwenye kikosi hicho na sasa jezi yake namba 23 na hatimye jezi hiyo aliikabidhi kwa beki kisiki Abdalah Shaibu (Ninja).
Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Sherehe zilianza mchana timu ya wanawake Yanga Princess ilipochuana na Moro Kombaini chini ya mwigizaji Wema Sepetu.
Yanga iliuandaa mchezo huo si tu kwa ajili ya burudani bali kuwachezesha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Baadhi ya wachezaji tangu wamesajiliwa hawajawahi kucheza mchezo wowote hivyo, Kocha Mwinyi Zahera alitarajia kuutumia mchezo huo kuwatazama na kutengeneza muunguniko mzuri wa kikosi chake cha kwanza.
Waliosajiliwa ni Mrisho Ngassa, Haritier Makambo, kipa Klaus Kindoki, Feisal Abdallah ‘Fei toto’, Mohamed Issa ‘Banka’ na Deus Kaseke ambaye yeye pekee tayari alishacheza katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Gormahia waliyofungwa 3-2.
Mchezo huo uliambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali kama vile Richi Mavoko, Afande Sele, Gigys Money na Msaga Sumu.

Leave a Comment