Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza bila mdhamini.


Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) imesema msimu ujao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara utaanza bila mdhamini mkuu wakati mipango ya kumpata mdhamini huyo ikiendelea kufanyika.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura ligi itaanza Agosti 22, mwaka huu kama kawaida chini ya wadhamini ya wenza Azam TV na Benki ya KCB.
Hata hivyo Wambura amesema bodi hiyo bado ipo kwenye mazungumzo na wadhamini waliomaliza muda wao ambao ni Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kuona kama inawezekana kuongeza mkataba wa udhamini katika ligi hiyo.
Wakati huo huo, Wambura amesema kuanzia msimu ujao wa ligi kuu, watoto chini ya umri wa miaka 18 wataingia viwanjani kutazama mechi za ligi hiyo kwa nusu ya kiingilio cha bei ya chini ya mtu mzima.

Leave a Comment