Rais Magufuli Aongoza Mamia Kuaga Mwili Wa Majuto, Dar.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amewaongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa Msanii wa vichekesho nchini Amri Athuman maarufu King Majuto, katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Viongozi wengine waliofika kumuuaga mwili wa mzee Majuto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole, Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zuberi, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhadi Salum na wengineo.
Mzee Majuto alifariki juzi Jumatano Agosti 8, 2018 saa mbili kamili usiku katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam na mwili wake kusafirishwa kwenda Tanga mjini ambako mazishi yatafanyika leo Ijumaa.

Leave a Comment