Idadi ya waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi nchini Indonesia yafikia 319.


Idadi ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na tetemeko la ardhi lilitokea zaidi ya wiki moja huko Lombok nchini Indonesia imeendelea kuongezeka na sasa imefikia 319.
Waziri wa Usalama wa Indonesia amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari kwamba, “Ripoti za hivi karibuni walizo nazo zinaonyesha kuwa, watu 319 wamepoteza maisha kutokana na tetemeko la ardhi”.
Tangazo hilo la serikali ya Indonesia limekuja siku yao chache tu baada ya kuelezwa kwamba, idadi ya watu waliopoteza maisha yao katika janga hilo la kimaumbile ni 164.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, bado kuna uwezekano wa kuongezeka idadi ya wahanga wa zilzala hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa, kuna watu ambao walitoweka na hawajulikani walipo hadi hivi sasa tangu baada ya janga hilo.
Msemaji wa idara ya kudhibiti majanga ya Indonesia amesema kuwa, nyumba nyingi zimeathirika vibaya, kufuatia tetemeko hilo la ardhi ambapo nyingi kati ya hizo zilijengwa kwa kutumia nyenzo duni.
Serikali ya Rais Joko Widodo wa Indonesia imesisitiza kuwa, inafanya jitihada za kutosha kunusuru maisha ya majeruhi sambamba na kuwapatia huduma na mahitaji ya lazima raia waliopoteza makazi yao kufuatia tetemeko hilo la ardhi.
Nchi ya Indonesia ni miongoni mwa mataifa ambayo hukumbwa na janga la tetemeko la ardhi kila mara na kusababisha maafa makubwa ya roho na mali za watu.

Leave a Comment