Rais wa Cameroon Paul Biya kubakia madarakani hadi 2025.


Rais wa Cameroon Paul Biya, ambaye yuko madarakani kwa karibu miaka 36 sasa, ametangaza kuwa atagombea muhula mwingine katika uchaguzi wa urais wa Oktoba 7 mwaka huu.
Huu utakuwa ni muhula wa saba wa miaka saba kugombewa na Biya mwenye umri wa miaka 85.
Biya aliandika ujumbe jana Ijumaa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijaii wa Twitter kwamba, “Wananchi wenzangu wa Cameroon na wale wanaoishi nchi za kigeni, tunajua changamoto ambazo tunakabiliana nazo Cameroon yenye umoja, usalama na amani. Nakubali kuitikia wito wenu, nitakuwa mgombea urais katika uchaguzi ujao wa urais.”
Biya ametoa tangazo hilo wakati huu ambapo machafuko yanaripotiwa kushtadi nchini humo, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakivitaka vyombo vya usalama kutotumia mbinu za ukatili kuzima malalamiko na maandamano ya wananchi wanaotaka majimbo yao yajitenge na serikali kuu ya Yaounde.

Leave a Comment