Kombe la Dunia: Neymar aiondoa Mexico, Brazil yatua robo fainali.


Neymar hakuchelea kung’ara kwenye mechi iliyotabiriwa kuwa na uwezo wa kukatiza maazimio ya Brazil kuliinua Kombe la Dunia mara yao ya 6 .
Nyota huyo amefanikiwa kuitingia timu yake Brazil 2-0 dhidi ya Mexico.
Mexico iliwatatiza mabeki wa Brazil Neymar hakuwa na uoga mbele ya lango na kila alipoona mwanya, alifyatua kombora.
Kufikia sasa Neymar ameandikisha shuti 23 dhidi ya wapinzani huku 12 mikwaju (12) ikizuiwa na wadakaji.
Nyota huyo wa PSG pia ameonyesha ukarimu wake kwa wenzake kwa kubuni fursa 16, zaidi ya wafungaji wengine wote Kombe la Dunia kufikia sasa.
Mexico ilianza mchuano ikijaribu mbinu ilizotumia dhidi ya Ujerumani za kufunga goli la mapema na kukusanyana mbele ya lango lao.
Ushirikiano bora kati ya kipa wa Brazil Alisson Becker na walinzi wake Thiago Silva pamoja na Miranda ulikatiza mipango ya Carlos Vela na Javier Hernandez marufu Chicharito.
Licha ya timu zote kutekeleza uvamizi, pande hizo zilienda mapumziko bila kufungana.
Brazil iliingia awamu ya pili kwa hamasa na kuhitaji tu dakika sita kuchukua uongozi.
Neymar, alijitengenezea nafasi nzuri karibu na lango na kuwa makini, punde tu baada ya mpira kuwavuka wote mbele ya lango, akiwemo kipa Ochoa, aliyezuia wafungaji wa Brazil, Neymar aliuwezesha mpira kufululiza na kutulia kwenye kamba.
Mexico iliwapa matumaini mashabiki wake kwa kufanya majaribio kwa lango la Brazil ili kusawazisha matokeo.

Leave a Comment