Azam FC Mabingwa Tena Kombe La Kagame Msimu Wa 2018, Baada Ya Kuichapa Simba 2-1 Uwanja. Wa Taifa.


Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kutetea tena ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki na Kati Maaarufu Kombe la Kagame baada ya kuwafunga Simba magoli 2-1 Mchezo uliomalizika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Shabani Idd Chilunda ambaye ameibuka Mfungaji bora wa Michuano hiyo baada ya kupachika jumla ya magoli 8 alianza kuwanyanyua mashabiki wa Azam FC kunako dakika ya 32 akimalizia mpira waa kona uliochongwa na kiungo mshambuliaji Ramadhani Singano ‘Messi’ akiukwamisha mpira kwa kichwa baada ya kuwazidi ujanja mabeki pamoja na mlinda mlango Dida.
Hadi timu zote zinaenda mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa goli hilo moja lililofungwa na Mchezaji Mpya wa Tenerrife ya nchini Hispania inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Shabani Chilunda.
Kipindi cha pili Simba waliingia kwa moto na kulisakama lango la Azam FC na katika dakika ya 65 Mshambuliaji Mpya Meddie Kagere aliisawazishia timu yake baada ya kufunga bao maridadi akimalizia pasi ya Rashid Juma aliyeingia kipindi cha pili huku likiwa goli lake la tano tangu ajiunge na Simba akitokea Gor Mahia ya Kenya .
Kapteni wa Azam FC Aggrey Morris alipingilia msumari wa pili kwa Simba dakika ya 70 kwa mpira wa Faulo alioupiga moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango Dida hii ni baada ya Paschal Wawa kumchezea rafu Messi na dakika ya 89 Azam FC walipata mkwaju wa Penalti baada ya Mohamed Husein kumchezea madhambi Frank Domayo na Kipa Razak aliweza kukosa Penalti hiyo kwa kupiga Mpira juu na kwenda nje.
Huku Nafasi ya tatu ikienda kwa timu ya Gor Mahia ambao wameshinda jumla ya magoli 2-0 dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Leave a Comment