WHO: Ebola inatishia maisha ya watu Congo DR.


Shirika la Afya Dunia (WHO) limetahadharisha kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mwishoni mwa safari yake ya siku mbili nchini Congo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirila la Afya Duniani, Tedros Adhanom amewaambia waandishi habari kuwa, ugonjwa wa Ebola unaenea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ametoa wito wa kuchukuliwa tahadhari zaidi kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Congo DR imesema kuwa, watu 14 wamepoteza maisha nchini humo kutokana na ugonjwa wa Ebola na kwamba kesi nyingine 14 zinazodhaniwa kuwa za ugonjwa huo zimesajiliwa.
Maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yalianza tarehe 8 Mei mwaka huu katika mji wa Bikoro kwenye mkoa wa Équateur huko kaskazini magharibi mwa Congo na baada yalihamia katika mji wa Mbandaka ambao ndio makao makuu ya mkoa huo.
Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2013 hadi 2016 ugonjwa huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 11 na 300 katika nchi za magharibi mwa Afrika.

Leave a Comment