Nchi 120 katika Umoja wa Mataifa zalaani mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina.


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio linaloulaumu na kuulaani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kufanya mauaji dhidi raia wa Kipalestina katika Ukanda wa Ghaza.
Katika kikao cha jana Jumatano, nchi 120 kati ya 193 za baraza hilo zilipiga kura ya ndio kuunga mkono azimio hilo lililowasilishwa na Kuwait na Uturuki kwa niaba ya nchi za Kiarabu na Kiislamu, huku nchi 8 zikipiga kura ya hapana na nchi 45 zikijizuia kulipigia kura azimio hilo.
Azimio hilo limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kutoa mapendekezo ndani ya siku 60, kuhusu njia za kuwadhaminia usalama na ulinzi wananchi madhulumu wa Palestina wanaoishi chini ya mzingiro wa utawala haramu wa Israel na ukaliwaji wa mabavu wa ardhi zao.
Kuwait na Uturuki zimewasilisha pendekezo hilo la kulaaniwa Israel katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa sababu ya kutumia risasi za vita dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza.
Hapo jana pia shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya jinai za kivita dhidi ya raia wanaoandamana huko katika Ukanda wa Gaza, Palestina.
Tangu tarehe 30 Machi mwaka huu hadi hivi sasa, wanajeshi katili wa Israel wameshaua shahidi Wapalestina wasiopungua 131 katika maandamano ya amani yaliyoanza wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa “Siku ya Ardhi” ambapo pia maelfu ya Wapalestina wamejeruhiwa.

Leave a Comment