Seneta nchini Nigeria atupwa jela miaka 14 kwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za serikali.


Seneta wa zamani wa Jimbo la Plateau Magharibi mwa Nigeria, Joshua Dariye, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa kiasi cha Naira bilioni 1.162 alipokuwa gavana wa jimbo hilo.

Ripoti zinasema kuwa, Dariye ambaye alihudumu cheo hicho kuanzia mwaka 1999 hadi 2007 alifanya ufisadi mkubwa wa fedha za jimbo hilo.
Awali Joshua Dariye alitiwa hatiani mwaka 2007 kwa makosa 23 yanayotokana na kosa hilo la ufisadi, na baadaye Mahakama Kuu ya Shirikisho chini ya Jaji Adebukola Banjoko imhukumu kifungo cha miaka miwili jela kwa kuvunja uaminifu.
Baadaye mahakama ya Nigeria ilimfungulia upya mashtaka na amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Mwanasheria wa Dariye, Paul Erokoro, amedai kuwa, mteja wake hakuelewa kosa hilo wakati lilipofanyika akiwa madarakani.
Aidha mwanasheria huyo ameongeza kuwa, mteja wake alikuwa akiwindwa na utawala wa kijeshi kwa miaka mingi na kwamba hakujua lolote kuhusu ufisadi wa fedha na mambo mengine yenye kuhusiana na jambo hilo.
Licha ya Rais Muhammadu Buhari kuahidi kwenye kampeni za uchaguzi kwamba atapambana na ufisadi nchini humo, lakini amekuwa akikosolewa kutokana na serikali yake kushindwa kuwachukulia hatua kali viongozi wengi wa serikali wanaohusishwa na ufisadi.

Leave a Comment