WHO yatuma dozi ya kwanza ya ugonjwa Ebola nchini Kongo DRC.


Shirika la Afya Duniani WHO limetuma shehena ya kwanza ya dozi 4,000 za chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Shehena ya chanjo hiyo ambayo inatumika kwa majaribio kwa mara ya kwanza iliwasilia nchini DRC jana Jumatano na ilianza kutegenezwa kufuatia mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi miaka miwili iliyopita.
Chanjo hiyo iliyotegenezwa na Shirika la Dawa la Merck, haijapata leseni badi lakini ilifanikiwa katika majaribio machache na ya awali wakati wa mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi ambapo watu 11,300 walipoteza maisha katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone kuanzia mwaka 2014-2016.
Maafisa wa afya wanasema wanaweza kutumia mkuripuko wa hivi sasa wa Ebola huko DRC kufanyia majaribio makubwa chanjo hiyo. WHO inasema tokea mwezi Aprili, Ebola imeua watu 20 nchini DRC.
Msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema shehena ya kwanza ya dozi 4,000 za chanjo imewasili Kinshasa na shehena ya pili ya dozi zingine 4,000 itatumwa nchini humo katika kipindi cha siku chache zijazo.

Leave a Comment