`Mbinu kukabili uvuvi haramu zimeshindwa’


Jamii ya wavuvi katika Kata ya Kisorya, Jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara, imesema kwamba mfumo unaotumiwa na serikali hivi sasa kukabili uvuvi haramu wa sumu umeshindwa.

Badala yake, jamii hiyo imeshauri kutumika mbinu zilizotumika wakati wa utawala wa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza wakati wa maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi katika Kata ya Kisorya (VFA), Msimu Mganga, alisema uvuvi haramu wa sumu unazidi kushamiri licha ya madai ya serikali kuwa inakabiliana nao kikamilifu.

Alisema mfumo wa sasa unaonekana kuchochea zaidi uvuvi haramu kutokana na viongozi hususani wa vijiji, kata na wilaya kuwakamata wahalifu na kisha kuwaachia pasipo kuwafikisha mahakamani.

Alifafanua kuwa hata pale ambapo raia wema wanajitolea kutoa taarifa za watu wanaofanya uvuvi haramu wa kutumia sumu, taarifa hizo huvuja na kuwafikia wahalifu na hivyo kuhatarisha maisha yao.

Aliongeza kwamba siku hizi watu wanafanya uhalifu wa wazi lakini wanaendelea kutamba mitaani, hali inayowakatisha tamaa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za siri.

Aliishauri serikali kuanza kuchunguza magari ya kubebea samaki ambayo yanapofika maeneo ya uvuvi hujaa samaki katika kipindi kifupi hali inayoonyesha kuwepo kwa uvuvi haramu wa kutumia sumu ambao huua samaki wengi.

Akizungumzia athari zinazotokana na uvuvi haramu wa kutumia sumu, Mganga alisema unasababisha samaki kuhamia katika maji marefu hali ambayo husababisha wavuvi wasio na mitaji mikubwa kushindwa kumudu shughuli za uvuvi.

 

CHANZO: NIPASHE

2 Comments

  1. KWANZA: ieleweke kuwa siku hizi za hivi karibuni uvuvi umechochewa sana na ubovu wa sera ya kurejesha maziwa na rasilimali nyingineza uvuvi kwa Serikali za mitaa ambazo zinaendeshwa chini ya mfumo wa “UBAZAZI wa Madiwani”. madiwani wengi katika maeneo ya uvuvi na rasilimali asili nyingine wametokana na wapiga kampeni za NICHAGUENI NITAWATETEA lakini pia watu hawa walikuwa kwa namna moja au nyingine wanajihusisha aidha na uvuvu haramu wenyewe au ndugu zao ambao wasingependa kuwataja kwa kuwa hawako COMMITTED ki-hivyo. lakini pia, wadiwani nao wanajua kuwa kuwataja wahusika ambao wanamkataba nao wanaweza kupoteza unga wa watoto wao au kufanyiwa chuki mtaani. PILI: Katika Halmashauri wako wataalam ambao katika hali ilivyo sasa HAWANA POWER pamoja na UTAALAM na MA-BOOK yao kama wanavyo ita wenyewe, wa kutatua TATIZO LA UVUVI HARAMU nA UVUVI HOLELA hata kwa nukta moja kwa 7bu zifuatazo:
    i. kutotengewa bajeti za kuendesha doria – wenye maamuzi ni walewale… ambao wanahofu ya kuvurugia mstari wa wapiga kura wao waliojipanga nyuma yao. hii pia inachangiwa na mkakati wao wa kuifanya jamii ibaki maskini na tegemezi ili waliopo madarakani waendelee kuabudiwa.
    ii. wataalam hawa hata kama ningekuwa mimi, wana hofu ya kudhurika wao pamoja na familia zao kutokana na wale wanaokamatwa, kufikishwa mbele ya vyombo vya dora au pia kuteketeza zana haramu kwa kuwa wapo palepale kijijini au mtaani.

    Ziko 7bu nyingine nyingi lakini ningedhani kuwa;- Serikali irejeshe usimazizi wa rasilimali hizi kwa SERIKALI KUU (Wizara)- wenyewe mtakuwa shahidi- zana haramu za uvuvi katika maeneo mengi nchini zimekuwa zikiteketezwa kutokana na doria zinazoendeshwa na ama Waziri au maafisa wake kwa kuwa wanavitendea kazi lakini wanafanya kazi hiyo bila hofu kwa kuwa hawaishi na waharifu karibu. hii pia itavunja mkataba kati ya waharifu na viongozi mapepe au viongozi vibaraka ambao pia wamekuwa hasara kwa kizazi kijacho na Taifa kwa ujumla.

    YAKO MENGI LAKINI TUONANE HAPA WAKATI MWINGINE

Leave a Comment