Rais mpya wa Misri aonyesha matumaini mema kwa wananchi wa Misri


Rais mpya wa Misri aonyesha matumaini mema kwa wananchi wa Misri
Mmoja kati ya wahariri wa masuala ya kisiasa nchini Misri amefurahishwa na hutuba ya Rais mteule wa Misri katika shereh za kuapishwa kwake na kusema: Rais huyo ameingiza matumaini mema kwa wamisri katika hutuba yake hiyo. 

Muhamamd Fathiy) muandishi na mchanbuzi wa masuala ya kisiasa nchini misri amesema: Muhammad Mursiy amekuwa Rais rasmi baada ya kuapishwa, na jeshi la nchi hiyo linapaswa kurejea makambini kutekeleza wadhifa wake wa kulinda mipaka ya nchi hiyo

Ama kuhusuuwezo wa Rais mpya wa nchi hiyo amesema: yeye anauwezo mkubwa wa kuiongoza nchi hiyo na kusimamia kikamilifu,na kusema hutuba alotoa baada ya kuapishwa iliamsha hisia na kumgusa kila mwananchi na kuweka matumaini mema kwa wananchi hao.

Rais huyo alisisitiza kazi za jeshi nakusema jeshi kazi yake ni kulinda mipaka na wananchi wa nchi hiyo na linapaswa kuzingatia suala hilo.

Leave a Comment