Ripoti: Asilimia 60 ya Wasaudi wanaishi chini ya mstari wa umasikini


Gazeti la Okaz Daily linalochapishwa kila siku nchini Saudi Arabia limeripoti kuwa asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo wanaishi chini ya mstari wa umasikini.
Ripoti ya gazeti hilo imesema kuwa Saudi Arabia inajipatia zaidi ya dola bilioni 400 kila mwaka kutokana na usafirishaji wa mafuta ghafi lakini licha ya utajiri huo, bado Wananchi wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha na kwamba asilimia kubwa ya watu ni masikini wa kupindukia.
Ripoti hiyo imekosoa watawala wa Riyadh kwa kutumia kiasi kikubwa cha pato la nchi kununulia silaha wakati nchi hiyo haiko vitani. Mwaka uliopita, Saudia ilinunua silaha zenye thamani ya dola bilioni 60 kutoka Marekani ambapo Washington ilikiri kuwa hiyo ndio biashara kubwa zaidi ya silaha iliyowahi kufanya na nchi moja.

Leave a Comment