Wazayuni wengine wawili wajichoma moto kulalamikia hali mbaya ya maisha Israel


Wapita njia wakijaribu kuzima moto uliokuwa ukiteketeza mwili wa Moshe Silman, aliyejichoma moto mjini Tel Aviv Juni 14, 2012, kulalamikia dhulma na hali mbaya ya maisha Israel. Silan alifaridi dunia siku sita baadaye.

Wazayuni wengine wawili wamejichoma moto katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Msemaji wa Jeshi la Polisi la utawala wa Kizayuni, Micky Rosenfeld amesema kuwa, Wazayuni wengine wawili walijichoma moto jana Jumatatu na kufanya idadi ya Wazayuni waliojichoma moto kulalamikia hali mbaya ya maisha kufikia wanne katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
Msemaji huyo amefafanua akisema, Muisraili mmoja mwenye umri wa takriban miaka 40 amejichoma moto kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu baada ya kujimwagia mada fulani na kujiwasha moto.
Kabla ya hapo pia, Muisraili mwingine mwenye umri wa karibu miaka 50 alijichoma moto mbele ya kituo kimoja cha polisi kwenye mji wa Ofakim kutokana na matatizo ya kifedha.
Suala la kujichoma moto Wazayuni kutokana na shida za maisha limekuwa ni jambo la kawaida hivi sasa.
Siku chache zilizopita, Mzayuni mmoja mwenye umri wa miaka 45 alijichoma moto katika kituo cha basi cha Yehud, yapata kilomita 15 mashariki mwa Tel Aviv. Madaktari walisema kuwa mwili wa Mzayuni huyo umeungua kwa asilimia 80.
Siku ya Jumamosi ya Julai 14 pia, Moshe Silman, mwenye umri wa miaka 57 alijimwagia mafuta ya taa na kujichoma moto mjini Tel Aviv kulalamikia dhulma kubwa aliyofanyiwa na viongozi wa utawala wa Kizayuni na matatizo ya maisha. Mzayuni huyo alifaridi dunia siku sita baadaye.

Leave a Comment