UN: Eritrea inaendeleza ukiukaji wa haki za binadamu


Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema leo kuwa serikali ya Eritrea inaendeleza vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuwashikilia watu bila kuwafikisha kortini. Navi Pillay amesema kuwa duru za karibu na Asmara zinasema kwamba kuna kati ya wafungwa 5000 na 6000 wa kisiasa katika jela za nchi hiyo. Pillay amesema pia kwamba serikali ya Eritrea bado inawatesa wafungwa pamoja na kubana uhuru wa kujieleza wa raia wake. Eritrea imekuwa chini ya utawala wa chama kimoja na imeongozwa na Rais Isaias Afewerki tangu ilipojipatia uhuru mwaka 1993 kutoka Ethiopia

Leave a Comment