Jumatano, Juni 20, 2012Siku kama ya leo miaka 137 iliyopita kisiwa cha Okinawa huko Japan kilidhibitiwa na jeshi la nchi hiyo.

Hata hivyo mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia kisiwa hicho cha kistratijia chenye ukubwa wa kilomita mraba 1250 kilikaliwa kwa mabavu na majeshi ya Marekani licha ya mapambano makali ya jeshi la Japan. Jeshi la Marekani liliondoka Japan mwaka 1958 lakini kisiwa cha Okinawa kiliendelea kudhibitiwa na Wamarekani. Askari wa Marekani walikomesha kukikalia kwa mabavu kisiwa hicho mwaka 1972 baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya pande hizo mbili.
Miaka 100 iliyopita msomi wa Poland kwa jina la Casimir Funk kwa mara ya kwanza kabisa alifanikiwa kugundua vitamin au virutubisho. Baada ya uhakiki mwingi Dakta Casimir Funk aligundua kwamba vyakula vinavyotumiwa na mwanadamu vina baadhi ya virutubisho (vitamin) ambavyo japokuwa ni vichache sana lakini vina udharura mkubwa katika ukuaji na usalama wa mwili na akaamua kuvipa jina la Vitamini.
Vitamin zina aina mbalimbali kama vitamin A, B, C, D na E na kila moja ina sifa za kipekee na matumizi ya aina yake katika mwili.
Na siku kama ya leo miaka 22 iliyopita mtetemeko mkubwa wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 7.3 kwa kipimo cha Rishta ulitikisa mikoa ya Gilani na Zanjan huko kaskazini mwa Iran na kusababisha hasara kubwa ya mali na nafsi.
Kitovu cha mtetemeko huo kilikuwa mji wa Rudbar na ulisababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 50 na kujeruhi wengine zaidi ya elfu 60. Mtetemeko huo ambao uliwalazimisha watu nusu milioni kuwa wakimbizi pia ulisababisha hasara kubwa za kiuchumi.

Leave a Comment