‘Nchi za Kiislamu zinapaswa kuwaunga mkono zaidi Wapalestina’


Naibu Waziri wa Masuala ya Mateka na Wapalestina Walioachiliwa Huru wa serikali ya Palestina amezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuwaunga mkono zaidi mateka wa Kipalestina na kuhakikisha wanatolewa katika jela za kutisha za utawala wa Kizayuni.
Muhammad al Katri amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al Alam akiweko mjini Ghaza na kuongeza kuwa, mateka wa Kipalestina wanakabiliwa na hali mbaya sana katika jela za Israel.
Amesema, mateka wa Kipalestina wanakabiliwa na hali mbaya mno hivi sasa wakiwa katika wiki ya nne ya kususia chakula na kadiri siku zinavyopita, ndivyo hali ya Wapalestina hao inavyozidi kuwa mbaya.
Hata hivyo amesema, msimamo wa mateka hao ni imara na wanakabiliana vilivyo na ukandamizaji wanaofanyiwa na askari magereza wa Israel.
Naibu Waziri huyo wa serikali ya Palestina ameongeza kuwa, ana matumaini harakati zinazofanyika huko Palestina na katika nchi za Kiarabu na Kiislamu za kuwaunga mkono mateka hao, zitaongezeka, kwani mateka hao wanapigania haki zao za kimsingi

Leave a Comment