Rais wa Namibia ataka uhusiano wa nchi yake na Iran uimarishwe zaidi


Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia ametaka uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uimarishwe zaidi.
Mwandishi wa Radio Tehran amemnukuu Rais Pohamba akisema hayo jana mjini Windhoek wakati alipoonana na mjumbe maalumu wa Rais Mahmoud Ahmadinejad na huku akigusia uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya Iran na Namibia amesema kuwa, nchi yake inaunga mkono misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kulinda haki yake ya kumiliki teknolojia ya amani ya nyuklia.
Rais Pohamba amesema, kumiliki nishati ya nyuklia ya matumizi ya amani ni haki ya nchi zote duniani.
Kwa upande wake, Bw. Hussein Amir Abdullahiyan mjumbe maalumu wa Rais wa Iran amemkabidhi Rais Pohamba, mwaliko rasmi kutoka kwa Rais Ahmadinejad wa kushiriki kwenye kikao cha wakuu wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungambana na Siasa za Upande Wowote NAM unaotarajiwa kufanyika hapa mjini Tehran mwezi Septemba mwaka huu.
Bw. Abdullahiyan pia amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza sana juu ya haja ya kustawishwa uhusiano kati yake na nchi za Afrika kadiri inavyowezekana na kwamba karibuni hivi Iran itafungua tena ubalozi wake nchini Namibia

Leave a Comment