Jumuiya ya ECOWAS


Jumuiya ya ECOWAS kutuma vikosi vya kijeshi nchini Mali na Guinea Bissau

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS itatuma vikosi vya kijeshi katika nchi zilizokumbwa na mapinduzi ya kijeshi za Mali na Guinea Bissau.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha dharura cha nchi wanachama wa ECOWAS kilichofanyika nchini Ivory Coast. Aidha viongozi wa ECOWAS wametoa taarifa inayowataka viongozi wa mapinduzi nchini Mali na Guinea Bissau warejee katika kambi zao za kijeshi na kukabidhi madarakani ya nchi kwa utawala wa kiraia.
Kadhalika viongozi wa Mali na Guinea Bissau wametakiwa na ECOWAS kuitisha uchaguzi wa Rais na Bunge katika kipindi cha mwaka mmoja ujao. Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho ametahadharisha kuhusiana na hatari ya ukosefu wa amani na uthabiti na kuenea ugaidi, uhalifu na jinai katika eneo magharibi mwa Afrika.

Na Salum Bendera

 

Leave a Comment