Serikali yahaha kusaka watumishi hewa


                                                                                       Wizara ya Fedha na Uchumi
kupitia Wizara ya Fedha imeanzisha zoezi la kuhakiki watumishi wake ili kukabiliana na wafanyakazi hewa katika wizara, taasisi za serikali na halmashauri zote nchini.

Katika kutekeleza zoezi hilo, Wizara ya Fedha, imesambaza waraka maalum katika ofisi zote za serikali ukitaarifu kuwa maofisa wake watapita kukagua vitambulisho vya wafanyakazi pamoja na hati za mishahara (salary slip) za miezi mitatu.

Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, aliithibitishia NIPASHE kuwepo kwa zoezi hilo na kwamba linawahusu watumishi wote wa serikali.

Alisema kwa muda mrefu ndani ya serikali na taasisi zake kumekuwepo na watumishi hewa ambao wanalipwa mishahara bila ya kufanya kazi.

Alifafanua kuwa wengi wa watumishi hao hewa waliishaacha kazi, wengine wamefariki, kustaafu ama kufukuzwa, lakini kwenye malipo wanaonekana kulipwa.

“Hili zoezi ni endelevu na litafanyika kwa nchi nzima ili kuhakikisha tatizo la watumishi hewa linakomeshwa ndani ya serikali,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

Leave a Comment