Leo ni Jumamosi tarehe 29 Mfunguo Nane Jamadul Awwal mwaka 1433 Hijiria inayosadifiana na terehe 21 April mwaka 2012 Miladia.


 

Leo ni Jumamosi tarehe 29 Mfunguo Nane Jamadul Awwal mwaka 1433 Hijiria inayosadifiana na terehe 21 April mwaka 2012 Miladia.
Miaka 33 iliyopita mwafaka na siku kama hii ya leo, Imam Khomein Mwenyezi Mungu amrehemu mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alitoa amri ya kuundwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah). Kwa mujibu wa amri hiyo wadhifa muhimu wa jeshi hilo ulikuwa ni kulinda na kuhifadhi Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya maadui wa ndani na nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Jeshi hilo lilianza kupambana na makundi yaliyo dhidi ya Mapinduzi katika maeneo tofauti nchini. Jeshi hilo pia lilionyesha uwezo wake mkubwa katika vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na dikteta Saddam Hussein wa Iraq dhidi ya Iran kwa lengo la kuyafuta Mapinduzi ya Kiislamu, sambamba na kuzima njama za maadui dhidi ya nchi hii.
Siku kama hii ya leo miaka 1182 iliyopita, Egbert Mfalme wa Kwanza wa Uingereza aliweza kuingia madarakani baada ya vita vya muda mrefu. Kabla ya hapo Uingereza ilikuwa ikiendeshwa na wafalme wa kitabaka ambapo ilikuwa imegawanywa katika sehemu kadhaa za kijiografia na kila mtawala akitawala eneo lake maalumu. Egbert aliyekuwa mfalme wa eneo lililokuwa Kusini mwa Uingereza ya sasa baada ya kupigana vita na watawala wa kitabaka na kuwalazimisha wamtii yeye, alipata fursa ya kuingia madarakani akiwa Mfalme wa Kwanza wa Uingereza na kuasisi nchini humo silsila ya utawala wa Wasaxoni wa Magharibi.
Miaka 159 iliyopita siku sawa na hii ya leo, alizaliwa katika mji wa Tabriz ulioko Kaskazini Magharibi mwa Iran alim na mjuzi wa lugha wa Kiirani Ayatullah Sheikh Muhammad Qasim Ardubadi. Baada ya kumaliza masomo yake ya kati alisafiri hadi Najaf ambapo alisoma kwa maulama mashuhuri wa mji huo. Msomi huyo mkubwa baada ya kufikia daraja ya ijtihadi alirejea mjini alikozaliwa na kuanza kufundisha huko. Ameandika vitabu kadhaa na miongoni mwake ni kitabu kiitwacho “As Shihabul Mubin fii I’jaazil Qur’an.” Alifariki dunia mwaka 1333 Hijiria.
Na miaka 154 iliyopita mwafaka na leo alifariki dunia mmoja wa wataalamu na malenga wa lugha ya Kiarabu Abdul Baqi bin Sulaiman Farooqi. Alikuwa na kipawa cha kusoma mashairi ya kuvutia tangu yu kijana. Aidha Abdul Baqi alikuwa mmoja wa wapenzi wa kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad (saw) ambapo aliyadhihirisha mapenzi yake hayo katika mashairi yake. Miongoni mwa vitabu vya msomi huyo ni pamoja na kitabu kiitwacho “Al Baqiyatus Swalihat.”

 

Leave a Comment