Watano wauawa katika mlipuko kwenye kambi ya jeshi Somalia


 


Watu watano wameuawa leo nchini Somalia baada ya mtu mmoja kujilipua mbele ya geti la kituo kimoja cha jeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu. Mlipuko huo wa leo asubuhi umetokea katika kambi ya jeshi ya Villa Baidoa katikati mwa Mogadishu.
Wakati hayo yakiripotiwa watu wasiopungua 9 wameuwa katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kijeshi zisizo na rubani za Marekani kusini mwa Somalia. Mashambulizi hayo yaliyofanywa karibu na mji wa Kulbiyow yamepelekea pia watu 28 kujeruhiwa. Katika siku za hivi karibuni mashambulizi ya ndege za Marekani zisizo na rubani yameongezeka nchini Somalia, ambapo makumi ya raia wa Somalia wameuawa.

Leave a Comment