Vitabu vya hotuba za hayati Mwalimu Nyerere vyazinduliwa


Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere

Vitabu vitatu vilivyoandikwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, vilizinduliwa jana katika viwanja vya Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Vitabu hivyo ni Uhuru na Mfumo mpya wa uchumi Duniani, Uhuru na Maendeleo na Uhuru na Siasa ya Kutofungamana.

Akifafanua baadhi ya vitu vilivyomo katika vitabu hivyo, Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Professa Issa Shivji, alisema vitabu hivyo vina hotuba za Mwalimu Nyerere ambazo alihutubia katika maeneo mbalimbali na kwa wakati tofauti.

“Vijana tusome vitabu vyote sita vya Mwalimu ili tujue kama sera na fikra zake zimepitwa na wakati ili kubishana naye kifikra na tusonge mbele kimaendeleo,” alisema.

Akizindua vitabu hivyo kwa niaba ya Mwalimu Nyerere Foundation, Mkuu wa Chuo cha Mwalimu Nyerere, alisema vitabu hivyo vina lengo la kuwafahamisha wananchi juu ya hotuba za Mwalimu na kila kitabu kina hotuba zaidi ya 30.

Hotuba zilizoko katika vitabu hivyo ni za kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 1999.

3 Comments

  1. goodluck kapyela says:

    nani wa kufanana na hayati baba wa taifa, mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amen

  2. ally says:

    watanzainia sisi sote ni ndungu kwa hiyo nawatakia heri chrismass.

  3. masta J J says:

    THANKS TO FATHER OF NATION.I WOULD LIKE TO READ THOSE BOOKS WHERE SHOULD I GET THEM?

Leave a Comment