‘Mashinikizo ya kigeni yanazuia kustawi uhusiano wa Iran na Misri’


‘Mashinikizo ya kigeni yanazuia kustawi uhusiano wa Iran na Misri’

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema madola ya kigeni yanaishinikiza Misri isiboreshe uhusiano wake na Iran.
Ali Akbar Salehi amesema pamoja na kuwepo mashinikizo hayo, Tehran na Cairo zina azma ya kuboresha uhusiano wao.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Iran inafahamu matatizo yanayoikumba Misri kuhusu suala hili. Ameongeza kuwa wakuu wa Misri wanataka wakati zaidi ili kuweza kuondoa mashinikizo ya kisiasa yaliyopo.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Nabil al Arabi alisema nchi yake inataka kufungua ukurasa mpya wa uhusiano na nchi zote. Uhusiano wa Iran na Misri uliharibika baada ya Cairo kutiliana saini mkataba wa Camp David na utawala haramu wa Israel mwaka 1978. Aidha uhusiano huo ulizorota zaidi baada ya Misri kumpa hifadhi mtawala wa kifalme aliyetimuliwa Iran Mohamad Reza Pahlavi. Baada ya kupinduliwa dikteta Mubarak mwezi Februari kumekuwepo na ishara za kuboreka uhusiano wa Cairo na Tehran.

Leave a Comment