Mafunzo ya semina ya vyombo vya habari-Desemba 12 2009


Hii ilikuwa semina ya kwanza we washiriki wa Al-Itrah Foundation na kushirikiana na waratibu ambao ni Nyota Foundation. Timu ya wanahabari huvutika  kuona uwezekano wa rasilimali watu wakitumia vipawa vyao katika suala zima la kuandaa habari kwa manufaa ya umma.

Waratibu wanayomatumaini na matarajio kwamba mambo haya yatakuwa yakiendelea kwa muda mrefu katika kuwaelimisha washiriki ikiwa  ni pamoja na kuwapatia zana husika kwa ajili ya maendeleo ya mbeleni.

 

 

 

 

 

 

 

Jumla kulikuwa na idadi ya washiriki 47 ikiwa ni pamoja na wanawake. semina hii ilidumu kwa karibu masaa 8 ikiendeshwa na al-Bayaan Media Group Company-DSM.

Masomo yaliyowasilishwa kwa wanasemina wakati wa warsha ni haya yafuatayo:

VIANZIO VYA KUANDAA KIPINDI

UTAYARISHAJI BORA WA KIPINDI.

MAHOJIANO

UWANDISHI WA SCRIPT

UTANGAZAJI BORA WA KIPINDI

UWANDAAJI mzuri WA RATIBA YA KIPINDI

Washiriki walikuwa na msisimko sana na warsha hiyo na kwamba wameomba kuendelea na mafunzo ya ndani kwa ajili ya Redio Maarifa na Runinga ya Ibn.

Leave a Comment